IQNA

Wayemen milioni 14 wanakabiliwa na njaa kutokana na hujuma ya Saudia

11:20 - November 08, 2018
Habari ID: 3471734
TEHRAN (IQNA) -Zaidi ya nusu ya Wayemen, takribani watu milioni 14, wanakabiliwa na baada la njaa kutokana na hujuma ya kijeshi inayoongozwa na Saudia dhidi ya taifa hilo masikini zaidi katika bara Arabu.

Katika taarifa wiki hii, mashirika 35 ya kutoa misaada yametoa wito wa kusitishwa vita dhidi ya Yemen ili kuokoa maisha ya mamilioni ya wananchi wasio na hatia.
Mashirika hayo ya kutoa misaada yameitaja jamii ya kimataifa ichukue hatua za kusitisha mapigano Yemen na pia kuzuia silaha zinazotumiwa dhidi ya watu wa Yemen.
Kati ya taasisi zilizotia saini taarifa hiyo ni pamoja na Oxfam, Action Against Hunger, Doctors of the World, CARE na taasisi kadhaa za Yemen.
Wakati huo huo kiongozi wa Harakati ya Ansarullah nchini Yemen amesema hujuma ya kijeshi dhidi ya nchi yake imeshika kasi zaidi baada ya utawala wa Rais Donlad Trump wa Marekani kutaka mazungumzo yafanyike kumaliza vita.
Akizungumza kwa njia ya Televisheni ya Al Masirah leo Jumatano katika mji mkuu wa Yemen, Sana'a, Sayyid Abdul-Malik Badreddin al-Houthi amesema kuna ushahidi kuwa maadui wanapanga kutekeleza hujuma kali dhidi ya Yemen chini ya usimamizi wa Marekani. Ameendelea kusema kuwa: "Njama zote dhidi ya Yemen zinatekelezwa na Marekani kwa kushirikiana na Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE). Aidha amesema Marekani ni mshirika mkuu wa jinai zinazotekelezwa na Saudia dhidi ya taifa la Yemen. Sayyid Badreddin al Houthi amewapongeza wapiganaji wa Yemen walio katika mstari wa mbele wa kulinda nchi yao. Ameongeza kuwa Wayemen wana haki ya kusimama kidete kujihami na kulinda uhuru wa nchi yao.
Inafaa kuashiria kuwa, Saudia ilianzisha mashambulizi dhidi ya Yemen mwishoni mwa mwezi Machi 2015 kwa lengo la kumrejesha madarakani Abdrabbuh Mansour Hadi, rais wa zamani wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kutoroka nchi. Hata hivyo Saudi Arabia na washirika wake wameshindwa kufikia malengo yao hayo huku wakisababisha maafa makubwa ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na kuwaua raia wasiopungua 15,000 wasio na hatia. Idadi kubwa ya watoto na wanawake ni miongoni mwa waliopoteza maisha katika vita dhidi ya Yemen vinavyoongozwa na Saudia kwa himaya ya madola ya Magharibi hasa Marekani na utawala haramu wa Israel.

3467164

captcha