IQNA

Kuwait yazindua Kituo cha Qur'ani cha Wasichana

15:57 - December 18, 2018
Habari ID: 3471776
TEHRAN (IQNA) – Kituo kipya cha Qur'ani kimefunguliwa kwa ajili ya washichana wenye umri wa miaka 15 hadi 19 katika mji wa Fahad al Ahmad mkoa wa Al Ahmadi nchini Kuwait.

Kwa mujibu wa Fahad al Janfawi, Mkurugenzi wa Masomo ya Kiislamu na Qurani katika Wizara ya Wakfu ya Kuwait, washichana watakaotumia kituo hicho ni kutoka mikoa ya Al Ahmadi na Mubarak Al Kabir.

Kituo hicho kinaanza shughuli zake Januari mwaka 2019. Al Janfai amesema ofisi ayke imeanzisha vituo 20 vya Qur'ani na masomo ya Kiislamu katika mikoa mbali mbali ya Kuwait na kwamba kuna vituo vingine 100 vya zamani ambavyo vimesajiliwa.

Amesema idara ya yake pia inapanga kufungua kituo maalumu cha kozi za Qur'ani kwa waliostaafu.

3772584

captcha