IQNA

China yapitisha sheria ya kuwalazimu Waislamu wafuate Usosholisti

12:15 - January 07, 2019
Habari ID: 3471799
TEHRAN (IQNA)- Utawala wa China umepitisha sheria mpya ya kuufanya Uislamu nchini humo uendane na itikadi ya 'Usosholisti wa Kichina' katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Kwa mujibu wa taarifa uamuzi huo umefikiwa katika mkutano baina maafisa wa serikali na taasisi nane zilizodaiwa kuwa za "Kiislamu" ambapo kulifikiwa mapatano kuwa Uislamu unaofuatwa nchini humo uende sambamba na Usosholisti wa Kichina.

Hakuna taarifa zaidi zilizotoelwa kuhusu kikao hicho au majina ya taasisi hizo nano zinazodaiwa kuwa za "Kiislamu" ambazo zimeidhinisha mpango huo.

Katika miaka ya hivi kairbuni China imekuwa ikitekeleza sera za makusudi za kuwalazimu Waislamu wafuate itikadi ya 'Usosholisit wa Kichina" jambo ambaloe limepelekea uhuru wa kuabudu nchini humo udidimei sana katika kipindi cha rais wa sasa Xi Jinping.

Utekeelzaji wa mafundisho ya dini ya Kiislamu ni marufuku katika baadhi ya maeneo ya China ambapo Waislamu wanaopatikana wakisali, wakifunga, kulea ndevu na kuvaa Hijabu hukabiliwa na tishio la kukamatwa na kuteswa.

Kwa mujibu wa wataalamu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa, Waislamu takribani milioni moja wa jamii ya Uighur wanashikiliwa katika kambi za kuwafunza Usosholisti wa Kichina na wanalazimishwa kwa kisingizio cha kukabiliana na ugaidi.

Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Kuangamiza Ubaguzi wa Rangi imesema imeandika ripoti kuhusu masaibu ambayo Waislamu wanakumbana nayo katika kambi hizo.

Uislamu ni kati ya dini tano ambazo zinatambuliwa rasmi na Chama cha Kikomunisti China ambapo kuna takribani Waislamu milioni 23 nchini humo.

Katika miaka ya hivi karibuni kumeongezeka sera za kuwakandamiza Waislamu katika nchi hiyo hasa katika jimbo la Xinjiang wenye Waislamu Zaidi ya milioni 10 kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi na misimamo mikali.

3467632

captcha