IQNA

Mahakama Uingereza yasema kupinga Uzayuni si kupinga Uyahudi

20:21 - January 15, 2019
Habari ID: 3471807
TEHRAN (IQNA)- Wazayuni wameshindwa kubatilisha uamuzi wa mahakama ya Uingereza ambaye imekataa kumfungulia mashtaka mwanaharakati wa Palestina kufuatia matamshi aliyotoa dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds mjini London mwaka 2017.

Mahakama Kuu ya Uingereza hivi karibuni imetupilia mbali kesi iliyowasilishwa na Kampeni ya Kukabiliana na Wapinzani wa Uyahudi (CAA) ambayo ilikuwa inalamikia uamuzi wa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP)  kutochukua hatua dhidi ya Nazim Ali. DPP amesema matamshi ya Nazim Ali hakutoa matamshi ya chuki katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds Juni 2017.

CAA ambayo lengo lake kuu ni kuutetea utawala wa Kizayuni wa Israel na kumtaja kuwa Mpinzani wa Uyahudi (anti-Semitic) kila anayeunga mkono Palestina na kupingiza Uzayuni, imedai kuwa Ali aliwatusi Wazayuni, makuhani wa Kizayuni na Bodi ya Mayahudi.

Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Uingereza ni ushindi muhimu kwa wanaharakati wanaounga mkono ukombozi wa Palestina kwa sababu ni hakikisho la uhuru wa maoni. Aidha uamuzi huo umepinga ile dhana ya kuwataka wanaopinga Uzayuni kuwa ni wapinzani wa Uyahudi.

Kumekuwa na dhana kuwa  “Uzayuni” na “Uyahudi”  ni kitu  lakini wasomi na wataalamu wa Kiyahudi wanasema kuwa, dhana na fikra kwamba maneno hayo yana maana moja si sahihi sawa. Pamoja na kuwa Wazayuni hujihesabu kuwa ni miongoni mwa Mayahudi, lakini Mayahudi wengi hujiweka mbali na fikra za Uzayuni.

3467702

captcha