IQNA

Qur'ani Tukufu Yasomwa Kila Siku Masaa 24 katika Msikiti wa Jamia Moscow, Russia

12:16 - January 22, 2019
Habari ID: 3471815
TEHRAN (IQNA)-Msikiti wa Jamia katika mji mkuu wa Russia, Moscow, umeanzisha mpango maalumu wa kusoma (qiraa) Qur'ani Tukufu kwa muda wa masaa 24 kila siku.

Qur'ani Tukufu Yasomwa Masaa 24 katika Msikiti wa Jamia Moscow, Russia
TEHRAN (IQNA)-Msikiti wa Jamia katika mji mkuu wa Russia, Moscow, umeanzisha mpango maalumu wa kusoma (qiraa) Qur'ani Tukufu kwa muda wa masaa 24 kila siku.
Kwa mujibu wa mpango huo ambao umeanza kutekelezwa mwaka huu wa 2019, wasomaji Qur'ani hupokezana zamu katika qiraa ambayo huendelea kwa masaa 24. Muda pekee ambao qiraa ya Qur'ani husitishwa msikitini hapo ni wakati wa sala tano za kila siku na sala ya Ijumaa. Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, qiraa hiyo huwa inarushwa hewani mubashara kupitia intaneti katika tovuti ya mihrabu.ru.
Msikiti wa Jamia wa Moscow ni msikiti mkubwa zaidi katika mji huo mkuu wa Shirikisho la Russia.
Jengo asili la msikiti huo lilijengwa mwaka 1904 na umekarabatiwa mara kadhaa tokea wakati huo. Septamba 11, mwaka 2011 jengo la kale la msikiti huo lilibomolewa na msikiti mpya ukajengwa na kufunguliwa rasmi Septemba 2015.
Msikiti huo ambao ulifunguliwa kwa mnasaba wa kuwadia Sikukuu ya Idul-Adh’ha una ghorofa sita na una uwezo wa kuchukua waumini elfu kumi. Uislamu ni dini ya pili yenye wafuasi wengi zaidi nchini Russia ambao idadi yao inafika milioni 25 kati ya watu wote milioni 144 nchini humo, na akthari ya Waislamu wanaishi katika eneo la Kaukasia ya Kaskazini.

3783320

captcha