IQNA

Waislamu wauawa baada ya Msikiti kuhujumiwa kwa gurunedi nchini Ufilipino

10:29 - February 01, 2019
Habari ID: 3471826
TEHRAN (IQNA)- Waislamu wasiopungua wasiopungua wawili wameuawa na wengine wanne kujeruhiwa kufuatia hujuma ya gurunedi dhidi ya msikiti kusini mwa Ufilipino.

Taarifa zinasema hujuma hiyo imejiri mapema Jumatano katika mji wa Zamboanga, ikiwa ni siku chache tu baada ya Kanisa Katoliki kushambuliwa karibu na kisia cha karibu. Matukio hayo mawili yamejiri pia siku chache tuu baada ya eneo lenye Waislamu wengine la Mindano kusini mwa Ufilipino kupiga kura ya kutaka mamlaka ya ndani.

Msemaji wa Jeshi huko Zamboanga Luteni Kanali Gerry Besana amethibitisha kuwa gurunedi ilirushwa ndani ya msikiti na Waislamu wawili wameuawa. Mkuu wa eneo hilo Mujiv Hataman amelaani vikali hujuma hiyo na kutoa wito kwa watu wa duni zote kuombea amani nchini humo.

Baraza la Maulamaa la Zamboanga limelaani hujkuma hiyo na kuitaja kuwa ya kishetani na iliyo dhidi ya ubinadamu.  Hakuna kundi lolote ambalo limedai kuhusika na hujuma hiyo. Jeshi la Ufilipino limetoa wito kwa jamii zote Mindani kuuungana na kujiepusha na uenezaji uvumi ambao unaweza kuvuruga utulivu.  Kundi la kigaidi la ISIS lilidai kuhusika na hujuma dhidi ya Kanisha katika eneo hilo la kusini mwa Ufilipino.

Hujuma za kigaidi dhidi ya maeneo ya ibada ya Waislamu na Wakristo nchini Ufilipino na yale yaliyozilenga nchi kama Indonesia katika miezi kadhaa ya hivi karibuni yanaonesha kuwa, harakati za makundi ya kigaidi zimeshamiri na kushika kasi zaidi katika eneo hilo. Suala hilo linazidisha udharura wa nchi na jumuiya za kikanda kuchukua tahadhari kubwa na kushirikiana katika kupambana na ukatili huo.  

3467835

captcha