IQNA

Morocco yajitenga na muungano wa Saudia uliovamia Yemen

14:50 - February 10, 2019
Habari ID: 3471836
TEHRAN (IQNA)- Morocco imejiondoa katika muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia katika vita dhidi ya Yemen.

Afisa mmoja wa serikali ya Morocoo ametangaza Alhamisi kuwa nchi yake haitashiriki tena katika uingiliaji kijeshi au vikao vinavyofanyika katika ngazi ya mawaziri katika muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudia dhidi ya taifa la Yemen

Habari ya kujitoa Morocco katika muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudia dhidi ya Yemen inatangazwa katika hali ambayo, mnamo tarehe 24 Januari, Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco Nasser Bourita katika mahojiano na Al Jazeera alisema kuhusu kushiriki nchi yake katika muungano huo kwamba: "Hivi karibuni, Morocco haijashiriki katika mazoezi mengi ya kijeshi na vikao vya mawaziri vya muungano wa kijeshi dhidi ya Yemen." Morocco tayari imeshamiwta nyumbani balozi wake aliyekuwa mjini Riyadh, Saudi Arabia kwa ajili ya mashauriano.

Inafaa kuashiria kuwa, Saudia ilianzisha mashambulizi dhidi ya Yemen mwishoni mwa mwezi Machi 2015 kwa lengo la kumrejesha madarakani Abdrabbuh Mansour Hadi, rais wa zamani wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kutoroka nchi.

Hata hivyo Saudi Arabia na washirika wake wameshindwa kufikia malengo yao hayo huku wakisababisha maafa makubwa ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na kuwaua raia wasiopungua 15,000 wasio na hatia.

Idadi kubwa ya watoto na wanawake ni miongoni mwa waliopoteza maisha katika vita dhidi ya Yemen vinavyoongozwa na Saudia kwa himaya ya madola ya Magharibi hasa Marekani na utawala haramu wa Israel.

3467883

captcha