IQNA

Sauti ya Adhana yasikika kote New Zealand kuonyesha mshikamano na Waislamu

23:04 - March 22, 2019
Habari ID: 3471885
TEHRAN (IQNA)-Katika kuonyesha mshikamano na uungaji mkono kwa Waislamu pamoja na familia za wahanga wa shambulio la kigaidi la Ijumaa iliyopita katika misikiti miwili ya Linwood na Al-Noor ya mji wa Christchurch nchini New Zealand, adhana imerushwa hewani kitaifa moja kwa moja katika televisheni na radio sambamba na misikiti yote ya nchi hiyo leo Ijumaa.

Hatua hiyo imekuja baada ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Bi.Jacinda Ardern kuamurisha kuwa Ijumaa ya leo adhana isomwe moja kwa moja kitaifa katika televisheni na radio sambamba na misikiti yote ya nchi hiyo. Aidha leo raia wa New Zealand wamenyamaza kimya kwa muda wa dakika mbili kama njia ya kutoa heshima yao kwa waliouawa katika hujuma misikitini. Halikadhalika misikiti yote ya nchi hiyo ilikuwa wazi Ijumaa kuanzia tangu asubuhi ili wasiokuwa Waislamu waweze kuitembelea na kujifunza kuhusu Uislamu.Sauti ya Adhana yasikika kote New Zealand kuonyesha mshikamano na Waislamu

Sala ya Ijumaa katika Bustani ya Hagley, Christchurch New Zealand

Halikadhalika Waziri Mkuu wa New Zealand amehudhuria Sala ya Ijumaa katika Bustani ya Hagley karibu na Msikiti wa al Noor akiwa amevalia Hijabu kama njia ya kuonyesha kufungamana na Waislamu nchini humo.

Wanaharakati katika mitandao ya kijamii nchini humo sambamba na kuanzisha kampeni ya vazi la hijab, wamewataka raia wa New Zealand kuzitembelea familia za wahanga wa shambulizi la kigaidi la Ijumaa iliyopita wakiwa wamevalia hijabu vichwani mwao.

Sauti ya Adhana yasikika kote New Zealand kuonyesha mshikamano na Waislamu

Waziri Mkuu wa New Zealand Bi. Jacinde Adern akiwasili kujumuika na Waislamu katika Sala ya Ijumaa katika Bustani ya Hagley,Christchurch, New Zealand

Katika shambulizi la kigaidi la Ijumaa iliyopita katika misikiti ya Linwood na al-Noor mjini Christchurch, watu 52 waliuawa shahidi na wengine 47 kujeruhiwa. Aliyefanya unyama huo ni Brenton Tarrant, gaidi mwenye chuki na Uislamu mwenye uraia wa Australia. Gaidi Tarrant ni mfuasi sugu wa  Rais Donald Trump wa Marekani ambaye ni mashuhuri kwa chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.

3799371

captcha