IQNA

Kiongozi wa Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Harakati ya Tauhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni chanzo cha uhasama wa Marekani

20:31 - April 03, 2019
Habari ID: 3471897
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwepo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika harakati ya Tauhidi (Kumpwekesha Mwenyezi Mungu) ni chanzo kikuu cha uhasama wa Marekani na vibaraka wake kama vile ukoo wa Aal Saud.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei aliyasema hayo leo asubuhi mjini Tehran wakati alipokutana na maafisa wa ngazi za juu wa  mfumo wa Kiislamu, mabalozi wa nchi za Kiislamu na wananchi wa matabaka mbali mbali kwa munasaba wa sherehe za kumbukumbu ya Kubaathiwa Mtumu Mtukufu wa Uislamu, Muhammad al Mustafa SAW. Ayatullah Khamenei ameendelea kuashiria maudhui ya Mabaath yaani kupewa Utume na Mwenyezi Mungu na kusema: "Kudhihiri Mitume wa Mwenyezi Mungu katika jamii mbali mbali ni tukio na harakati kubwa ya kuelekea katika 'Tauhidi  na Ibada' na 'Kujiepusha na Taghuti' na kuongeza kuwa: "Taghuti kwa hakika ni ile harakati iliyo kinyume cha Tauhidi na misdaki yake katika zama zetu za leo ni marais wa Marekani na baadhi ya nchi."

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameendelea kusema kuwa: "Hujuma za utawala wa Kizayuni katika kipindi cha miaka mingi mutawalia ni mfano wa wazi wa Taghuti anavyoeneza na hatua ya Wapalestina na Hizbullah ya Lebanon kukabiliana na hujuma hizo na pia kujihami kutakatifu Iran katika kipindi cha miaka minane ni misdaki ya wazi ya Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu."

Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni muendelezo wa Kubaathiwa Mtume Mtukufu wa Uislamu na kuongeza kuwa kuhasimiwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ni sawa na yale makabiliano ya kambi ya Taghuti na kambi ya Tauhidi. Ameongeza kuwa si sahihi kusema tusiwe na uhasama kwani mrengo wa Taghuti unapingana na msingi pamoja na utambulisho wa Tauhidi na kwa hivyo Marekani na watumwa wake kama vile ukoo wa Aal Saudi, unaotawala Saudi Arabia, hawataridhika isipokuwa katika kukabiliana na harakati ya Tauhidi.

Kiongozi Muadhamu ameendelea kusema kuwa: "Iwapo taifa la Iran litaendelea na harakati zake, bila shaka na kwa yakini litapata ushindi katika makabiliano na adui, yaani Marekani na vibaraka wake."

Kwingineko katika hotuba yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewasisitizia wakuu wa nchi kuwa kazi muhimu sasa ni ukarabati na ujenzi mpya wa maeneo yaliyoharibiwa katika mafuriko yalioyokumba maeneo mengi ya Iran na pia kuwalipa fidia waathirika.

Kiongozi Muadhamu amesema katika maafa hayo ya mafuriko hivi karibuni Iran, wananchi wamonyesha moyo mzuri wa mashikamano na kujitolea kuwasaidia wenzao. Aidha amesema maafisa wa nchi nao pia wamepata uungaji mkono wa wananchi katika kuwasiadia waathirika na kwa mshikamano huo waliweza kuchukua hatua za awali kwa mafanikio.

3800802

captcha