IQNA

Tarjuma ya Qur'ani kwa lugha ya Asante Twi ya Ghana

13:15 - May 01, 2019
Habari ID: 3471937
TEHRAN (IQNA) – Tarjuma ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Asante Twi imezinduliwa eneo la Kumasi, kusini mwa Ghana ili kuwawezesha wanaozungumza lugha hiyo kusoma kitabu hicho kitukufu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, tarjuma hiyo imetayarishwa na mwanazuoni maarufu wa Kiislamu Sheikh Harun Nkansha Agyekum ambaye amechukua muda wa miaka ya 40 kuandika tarjuma hiyo kutoka lugha ya Kiarabu.

Akizungumza katika uzinduzi wa tarjuma hiyo, Imamu Mkuu wa Zamani wa Jeshi la Ghana Luteni Kanali Umar Sanda Ahmed amempongeza Sheikh Nkansah kwa mradi huo muhimu na amemuomba Allah SWT ambariki kwa kazi yake hiyo yenye thamani kubwa.

Naye Imamu wa Eneo la Ashanti, Sheikh Abdul Mumin, ametoa wito kwa Waislamu kusoma Qur'ani Tukufu ili waweze kufahamu mafundisho yake.

Aidha amemtoa wito wa kuishi kwa maelewano wafuasi wa dini zote nchini Ghana.

Lugha ya Asante Twi inazungumzwa na watu wa jamii ya Ashanti wanaokadiriwa kuwa milioni 2.8.  Kiashante ni kati ya lahaja tatu za lugha ya Akan ya Afrika Magharibi. Lugha ya Asante Twi inazungumza katika eneo la Ashanti nchini Ghana.

3468413

captcha