IQNA

Maonyesho ya Qur'ani Tehran kushirikiana na taasisi za Qur'ani duniani

10:20 - May 16, 2019
Habari ID: 3471959
TEHRAN (IQNA)- Mkurugenzi wa Kitengo cha Kimataifa cha Maonyesho ya 27 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran amesema kushirikiana na taasisi za kimataifa za Qur'ani ni moja kati ya malengo muhimu ya maonyesho ya mwaka huu.

Dkt. Mahmoud Vaezi Mkurugenzi wa Kitengo cha Kimataifa cha Maonyesho ya 27 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran ameyasema hayo katika mahojiano na IQNA na kuongeza kuwa, katika maonyesho ya mwaka huu, badala ya kuziomba serikali zishiriki, taasisi za Qur'ani kutoka nchi mbali mbali zimealikwa kushiriki.

Amesema kati ya taasisi muhimu zilizoshirikia ni Taasisi ya Yayasan Restu ya Malaysia na Chuo Kikuu cha Ez Zitoun cha Tunisia, ambacho ni kati ya vyuo vikuu vikongwe zaidi duniani.

Vazezi ameongeza kuwa, Pakistan ni mgeni maalumu wa maonyesho ya mwaka huu huku akiongeza kuwa nchi kadhaa pia zinashiriki. Kitengo cha Kimataifa cha Maonyesho ya 27 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran lilizinduliwa rasmi Jumatatu jioni. Nchi zingine ambazo zimeshiriki katika maonyesho ya mwaka huu ni pamoja na Bahrain, Palestina, Nigeria, Yemen, Cameroon, Tajikistan, Azerbaijan, Afghanistan, Oman na Ivory Coast.

Maonyesho ya 27 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran yanaendelea katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini MA na yanatazamiwa kuendelea hadi 24 Mei. Maonyesho hayo hufanyika kila mwaka katika kipindi cha siku 20 za kwanza za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

3811674

captcha