IQNA

Rais Magufuli wa Tanzania ahudhuria mashindano ya Qur’ani

12:27 - May 21, 2019
Habari ID: 3471966
TEHRAN (IQNA)- Rais John Magufuli wa Tanzania amehuhdhuria Mashindano ya Kimataifa ya Kusoma na Kuhifadhi Qur’ani yaliyofanyika Jumapili Mei 19.

Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Magufuli amesema amevutiwa sana na qiraa au usomaji wa Qur’ani aktika mashindano hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Aidha ametoa wito wa kuongeza idadi ya nchi zinazoshiriki kutoka 18 hadi nchi zote za bara la Afrika. Rais Magufuli ameseam wakati aya za Qur’ani zilipokuwa sikisomwa, Mufti wa Tanzania alikuwa akijitahidi kumtafsiria maana kwa sababu alikuwa haelewi kinachosomwa zaidi ya kusikia sauti nzuri.

“Nigekuwa mtoa maksi wote wangeshinda. Napenda kuwapongeza waandaaji wa mashindano ya Qur’ani na kwa wingi wa watu waliojitokeza katika mashindano  haya Mungu atusamehe dhambi zetu,” alisema Rais Magufuli.

Marais wastaafu wa wa Tanzania, Jakaya Kikwete na Ally Hassan Mwinyi pia walihudhuria mashindano hayo. Waziri Mkuu wa Tazania Kassim Majaliwa pia alihudhuria mashindano hayo ya Qur’an Tukufu ambayo pia yalihudhuriwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry bin Ally.

Mshindi katika kitengo cha kuhifadhi Qur’ani kikamilifu alikuwa ni Mohamed El Moujabba Diallo wa Senegal  ambaye alipata zawadi ya Shilingi (Tz) milioni 20.

captcha