IQNA

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu

Saudia ilinde usalama na hadhi ya Mahujaji

18:07 - July 03, 2019
Habari ID: 3472031
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema serikali ya Saudi Arabia ina wajibu na majukumu mazito ya kulinda usalama wa mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu na hadhi yao bila ya kueneza anga ya kipolisi.

Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu  ameyasema hayo mapema leo mjini Tehran katika hadhara ya maafisa wa Hija nchini Iran. Katika kikao hicho ambacho hufanyika kila mwaka kabla ya msafara wa kwanza wa Wairani wanaoelekea Hija, ameashiria masuala muhimu ya kisiasa yaliyomo kwenye ibada ya Hija kama kulindwa umoja, kuwatetea watu wanaodhulumiwa na kujitenga na washirikina na kusisitiza kuwa: “Umoja, kuwatetea wanaodhulumiwa kama taifa la Palestina na watu wa Yemen au kujitenga na kujiweka mbali na washirikina yote ni mambo ya kisiasa yanayooana na mafundisho ya Uislamu; kwa msingi huo masuala ya kisiasa ya ibada ya Hija ni wajibu wa kidini na kiibada. “

Ayatullah Khamenei amesema, sambamba na harakati za kisiasa za kidini, kuna hatua za kisiasa zisizo za kidini na za kishetani kama vile kusema kuwa, Waislamu wasieleze upinzani wao dhidi ya Marekani wakati wa ibada ya Hija au kwamba wasitangaze kujibari na kujitenga na washirikina. 

Amesisitiza kuwa: "Kujitenga na washirikina ni faradhi na wajibu wa Kiislamu na jambo la lazima, na kwa sababu hiyo tunasisitiza kuwa, suala hilo linapaswa kufanyika kila mwaka tena kwa njia bora zaidi."

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria uhasama mkubwa wa Marekani na mabeberu wengine dhidi ya masuala ya Kiislamu na kusema: Hujuma ya kutisha ya kisiasa, kijamii, kiutamaduni, kiuchumi na kiusalama ya mabeberu wa kimataifa dhidi ya mataifa ya Waislamu ni kielelezo cha uadui wao mkubwa dhidi ya mafundisho ya Kiislamu.

Amesema kuwa maarifa ya Kiislamu yanapinga sera za kidhalimu za mabeberu na kuongeza kuwa, kushikamana kwa jamii za Kiislamu na misingi na sheria za Uislamu na kutosalimu amri mbele ya madhalimu ndiyo siri ya ushindi, maendeleo, mafanikio na uokovu wa Umma wa Kiislamu. 

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, mustakbali wenye maendeleo na izza ya Waislamu vinahitajia kufanya bidii, jihadi na ushirikiano na kuongeza kuwa, kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu, maadui wenye tabia za kinyama wa taifa la Iran na Umma wa Kiislamu hatimaye watalazimika kuupiga Uislamu magoti.

3824086

captcha