IQNA

Mahakama ya Federali ya Nigeria imeiruhusu serikali kuiweka Harakati ya Kiislamu katika orodha ya makundi ya kigaidi

12:21 - July 28, 2019
Habari ID: 3472057
TEHRAN (IQNA) - Mahakama ya Federali ya nchini Nigeria imeiruhusu serikali kuiweka Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo katika faharasa ya makundi ya kigaidi.

Dayo Apata Naibu Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Nigeria amethibitisha kuwa mahakama hiyo imetoa dikri na kuiruhusu serikali kupiga marufuku shughuli za Harakati ya Kiislamu ya Nigeria. Ofisi ya Sheikh Ibrahim Zakzaky Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imetoa radiamali kwa hatua hiyo ya mahakama ya Federali na kueleza kuwa kulikuwepo na nmpango wa kupiga marufuku shughuli za harakati hiyo tangu mwaka 2015 na kutolewa hukumu hiyo pia ni jambo lililotarajiwa.

Wakati huo huo wafuasi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria wamefanya maandamano huko Abuja mji mkuu wa nchi hiyo wakisisitiza kuachiwa huru Sheikh Ibrahim Zakzaky kiongozi wa harakati hiyo. Sheikh Zakzaky bado yuko jela licha ya mahakama nchini humo mwaka 2015 kuamuru kuachiwa huru mwanazuoni huyo. Harakati ya Kiislamu ya Nigeria ambayo ni mwakilishi wa Waislamu wa Kishia nchini humo imetangaza kuwa itaendelea kufanya maandamano hadi hapo Sheikh Ibrahim Zakzaky mwanazuoni mkubwa wa Kiislamu na mwasisi wa harakati hiyo atakapoachiwa huru.

http://parstoday.com/

 

captcha