IQNA

15:13 - July 28, 2019
News ID: 3472058
TEHRAN (IQNA)- Kongamano la kimataifa la masomo ya Qur'ani limefanyika katika mji wa Tangier nchini Morocco.

Kwa mujibu wa taarifa, kongamano hilo limewaleta pamoja wataalamu kutoka nchi kadhaa na lilianza Alhamisi na kumalizika Ijumaa. Washiriki katika kongamano hilo waliwasilisha makala zao kwa lugha za Kiarabu, Kiingereza na Kifaransa.
Kongamano hilo liliandaliwa na Jumuiya ya Masomo ya Qur'ani Morocco na kufanyika katika tawi la Morocco la Chuo Kikuu cha New England cha Marekani.
Kati ya mada muhimu zilizojadiliwa katika kongamano hilo ni 'Qur'ani na Dini Zinginezo', 'Tarjuma na Tafsiri ya Qur'ani', Mbinu za Masomo na Tafsiri ya Qur'ani n.k.

3830007

Name:
Email:
* Comment: