IQNA

Rais Bashar al Assad wa Syria ashiriki katika Sala ya Idul Adha + PICHA

12:36 - August 11, 2019
Habari ID: 3472078
TEHRAN (IQNA) – Rais Bashar al Assad wa Syria leo asubuhi ameshiriki katika Sala ya Idul Adha iliyofanyika katika Msikiti wa al-Afram mjini Damascus.

Rais al Assad ameshiriki katika Sala akiwa ameandamana na Waziri wa Wakfu, Mufti Mkuu wa Syria, maafisa wa ngazi za juu serikalini, wabunge, maulamaa na raia wa kawaida.

Sala hiyo ya Idi iliswalishwa na Sheikh Hassan Awad ambaye katika hotuba yake ameashiria fadhila za Idul Adha na darsa na ibra zipatikanazo katika siku hii zikiwa ni pamoja na subira katika wakati mgumu na kujitolea kulinda heshima na usalama wa nchi.

Kwa mnasaba wa Siku Kuu ya Idul Adha, kutakuwa na siku tano za mapumziko Syria kuanzia jana Jumamosi.

Katika baadhi ya nchi duniani leo imesaliwa Sala ya Idul Adha huku baadhi ya nchi zikitazamiwa kusimamisha Sala ya Idul Adha kesho Jumatatu 12 Agosti 2019 kwa kutegemea fiqhi ya mwezi mwandamo ambayo inafuatwa na Waislamu wa kila eneo.

Rais Bashar al Assad wa Syria ashiriki katika Sala ya Idul Adha

Rais Bashar al Assad wa Syria ashiriki katika Sala ya Idul Adha

Rais Bashar al Assad wa Syria ashiriki katika Sala ya Idul Adha

Rais Bashar al Assad wa Syria ashiriki katika Sala ya Idul Adha

3834108

Kishikizo: iqna syria idul adha
captcha