IQNA

Nigeria yakiri kuwazika Waislamu katika kaburi la umati

14:28 - April 13, 2016
Habari ID: 3470245
Serikali ya Nigeria imekiri kuwazika Waislamu 347 wa madhehebu ya Shia katika kaburi la umati mwezi Desemba mwaka 2015.

Katibu wa serikali ya jimbo la Kaduna Balarabe Lawal ametoa tangaza hilo Jumatatu katika kikao cha kuchunguzi mauaji hayo.

Ikumbukwe kuwa kati ya Desemba 12-14 mwaka 2015, Jeshi la Nigeria liliwashambulia wafuasi wa Harakati ya Kiislamu Nigeria IMN katika mji wa Zaria jimboni Kaduna kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Jeshi lilidai kuwa wafuasi wa IMN walikuwa na jama ya kutoaka kumuua Mkuu wa Jeshi la Nigeria, madai ambayo yamekanusha vikali na wafuasi wa harakati hiyo.

Katika ushahidi wake, Lawal amekiri kuwa wanajeshi 40 wa Nigeria walisimamia zoezi la kuzikwa kwa umatu Waislamu 347 waliouawa na jeshi la nchi hiyo.

Muhammad Namadi Musa, Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Wafuasi wa Dini Mbalimbali amesema kutangazwa rasmi kuwepo kaburi hili la umati ni ushahidi wa wazi kuwa mamia ya Waislamu waliuawa Desemba mwaka jana wakati jeshi la Nigeria lilipowashambulia Waislamu mjini Zaria. Katika tukio hilo, jeshi la Nigeria liliwafyatulia risasa wafuasi wa harakati hiyo inayoongozwa na Sheikh Ibrahim Zakzaky ambaye sasa anashikiliwa na jeshi la nchi hiyo akiwa na majeraha na risasi mwilini.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limetoa wito wa kufanyika uchunguzi kuhusu mauaji ya Waislamu hao nchini Nigeria.

Taasisi hiyo ya kimataifa imesisitiza kuwa, matamshi yaliyotolewa na afisa mmoja wa serikali ya Nigeria aliyesema kuwa maiti 347 za wanachama wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imezikwa kwa siri, yanapaswa kuchunguzwa na wahusika wa uhalifu huo wachukuliwe hatua.

Wataalamu wa Amnesty International wanasema kaburi hilo la umati linapaswa kulinda baada ya maiti zilizomo kufanyiwa uchunguzi kamili wa kisheria.

/3488164

captcha