IQNA

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi Iran kuandaa mashindano ya Qur'ani

10:11 - January 23, 2011
Habari ID: 2068947
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC nchini Iran limepanga kuanzisha mashindano ya kitaifa ya Qurani kuanzia Februari 13-16 mjini Tehran.
Kwa mujibu wa Muhammad Ali Asudi, Mkuu wa Masuala ya Utamaduni katika Idara ya Mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika IRGC amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa mashindano hayo yatawashirikisha maafisa 654.
Amesema mashindano hayo yatakuwa na viwango kadhaa vikiwemo vya kuhifadhi juzuu, 5,10,15, 20 na Qur'ani nzima. Aidha kutakuwa na mashindano ya utafiti wa Qur'ani, tarteel na adhana.
Amesema mashindano hayo yanafanyika kwa lengo la kuimarisha kiwango cha ujuzi na umahiri wa makarii na mahafidh.
Akiashiria shughuli za Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, ameongeza kuwa warsha za Qur'ani zitafanyika pembizoni mwa mashindano hayo ili kuimarisha uwezo wa washiriki katika ufahamu wa Qur'ani.
734659
captcha