IQNA

Kitengo cha utafiti kiongezwe katika mashindano ya Qur'ani

13:59 - January 26, 2011
Habari ID: 2070203
Kitengo cha utafiti wa Qur'ani kinapaswa kuwa kitengo kikuu katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya wanachuo Waislamu.
Hayo yamesemwa na Hujjatul Islam Mohammadi Mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu na Mkuu wa Shirika la Awqaf na Misaada la Iran.
Akizungumza na mwandishi wa IQNA amesema Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu yalikuwa na idadi kubwa ya wawakilishi kutoka pembe zote za dunia jambo ambalo limeinua kiwango cha mashindano hayo.
Akiashiria vitengo mbalimbali katika mashindano hayo, Hujjatul Islam Mohammadi amesema kuwa kitengo cha utafiti kuhusu misingi na mafundisho ya Qur'ani Tukufu ni kitengo ambacho kinapaswa kuongezwa katika mashindano hayo.
“Wanachuo Waislamu wanapaswa kujifunza kwa kina mafundisho ya Qur'ani”, ameongeza.
Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Wanachuo Waislamu yalifanyika Januari 9-11 katika mji wa Mash'had kaskazini mashariki mwa Iran na kuwashirikia wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka nchi 40 duniani.
735561
captcha