IQNA

Wawakilishi wa Ayatullah Khamenei waelekea Madina

22:04 - January 29, 2011
Habari ID: 2072086
Wawakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei wameelekea katika mji mtakatifu wa Madina kuwasilisha salamu za rambirambi za Kiongozi Muadhamu kufuatia kifo cha Allamah Sheikh Muhammad Ali al Amri ambaye alikuwa miongoni mwa wanazuoni wakubwa wa madhehebu ya Shia nchini Saudi Arabia.
Kituo cha habari cha ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kimeripoti kuwa Ayatullah Ahmad Jannati na Hujjatul Islam Marvi wametumwa na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Khamenei kwenda mjini Madina kwa shabaha ya kuwasilisha rambirambi za kiongozi huyo kwa familia ya Ayatullah al Amri na kushiriki katika majlisi ya kumuombea rehma na maghufira mwanazuoni huyo.
Ayatullah Muhammad Ali al Amri alikuwa akitambuliwa kuwa ndiye kiongozi wa kiroho wa Waislamu wa madhehebu ya Shia wa Saudi Arabia kutokana na nafasi yake ya juu ya kielimu na kiakhlaki.
Ayatullah Muhammad Ali al Amri ambaye amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90 alifungwa katika jela za utawala wa Saudi Arabia kwa kipindi cha miaka 45 kutokana na kufuata madhehbu ya Watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad (saw). 738401

captcha