IQNA

Mascow, mwenyeji wa maonyesho ya Kisanii kuhusu Qur'ani Tukufu

17:06 - August 16, 2011
Habari ID: 2171700
Maonyesho yanayoonyesha kazi za kisanii za Wasil Hananov, msanii wa Kirussia zenye maudhui mbalimbali ya Qur'ani Tukufu yanaendelea huko katika mji mkuu wa nchi hiyo Moscow.
Maonyesho hayo ambayo yamepewa jina la Wahyi yanaonyeshwa katika jumba la maonyesho ya kazi za sanaa la Inzhir. Msanii huyo amesema kuwa lengo la kuandaa maonyesho hayo sio kwa maslahi yake binafsi bali ni kuwafanya watu watafakari na kuizingatia Qur'ani Tukufu pamoja na malengo ya maisha yao humu duniani na huko Akhera.
Hananov ambaye ni mwanakaligrafia na mchoraji mashuhuri wa Russia ambaye pia ni mwanachama wa Jumuiya ya Wasanii wa nchi hiyo alianza kuzingatia Qur'ani Tukufu katika kazi zake za kisanii mwaka 1990.
Hivi karibuni msanii huyo pia aliandaa maonyesho mengine yanayohusiana na Qur'ani Tukufu katika jumba la maonyesho ya mambo ya kale mashariki mwa Moscow.
Maonyesho ya sasa yanatazamiwa kumalizika tarehe 15 Septemba. 843836
captcha