IQNA

Kikao cha tano cha Baraza Kuu la Jumuiya ya Ahlul Beit (as) chafunguliwa

14:29 - September 11, 2011
Habari ID: 2184946
Kikao cha Tano cha Baraza Kuu la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Beit (as) kimefunguliwa leo Junapili mjini Tehran kwa hotuba ya Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kikao hicho ambacho kinawashirikisha wasomi, wanazuoni na wanafikra mashuhuri wa Kishia zaidi ya 500 kutoka pembe zote za dunia, kitaendelea hadi tarehe 14 Septemba.
Kabla ya hotuba ya ufunguzi wa kikao hicho Ayatullah Muhsin Mujtahid Shabstari, mwanachama wa Kamati Kuu ya Ahlul Beit (as) na vilevile Ayatullah Mahdi Kani, Mkuu wa Baraza la Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran wamehutubia washiriki wa kikao hicho. Kikao cha kwanza cha Baraza la Ahlul Beit kilifanyika mjini Tehran miaka 22 iliyopita ambapo uamuzi wa kulifanya kuwa la kimataifa ulichukuliwa baada ya kuafikiwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Baraza hilo hutekeleza shughuli zake kama shirika la kimataifa lisilokuwa la kiserikali na mkutano wa wajumbe wake hufanyika mara moja kila baada ya miaka minne. 858189
captcha