IQNA

Ayatullah Khamenei:

Mabeberu wanatumia mbinu ya kuharibu maadili

22:07 - September 20, 2011
Habari ID: 2190919
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Ali Khamenei amesema kuwa mabeberu wanatumia mbinu ya kuchafua amani ya kijamii, kimaadili na kiroho kwa ajili ya kukabiliana na mataifa yanayojitawala.
Ayatullah Khamenei ameyasema hayo leo katika hadhara ya wafanyakazi na makamanda wa jeshi la polisi la Iran na kulitaja jeshi hilo kuwa ni walinzi wa amani na utulivu wa wananchi. Ameongeza kuwa wanasiasa wa kambi ya ubeberu wanaeneza dawa za kulevya na tabia ya kuchupa mipaka ya maadili na kudhoofisha nguzo za akhlaki kwa lengo la kukabililiana na mataifa yanayojitawala.
Ayatullah Khamenei amesema kuwa mapambano sahihi na ya kina dhidi ya ufuska yanahitaji kufutilia mbali mambo yote yanayoweza kuwa na madhara kwa jamii.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, jeshi la polisi linapaswa kuwa dhihirisho la nguvu na nidhamu na kielelezo cha huruma, rehma na upendo katika jamii. Ameashiria maendeleo makubwa ya jeshi la polisi hapa nchini na kusema kuwa, kuna uwanja nzuri wa kuwepo ustawi na maendeleo zaidi, suala ambalo haliwezekani bila ya kuwa na elimu, uzoefu, uhakiki, taamuli na kutumia vipawa na uwezo wote.
Ayatullahil Udhmaa Ali Khamenei ameongeza kuwa fahari ya Iran imo katika azma imara ya vijana na wasomi wa nchi hii ambayo kwa baraka zake Allah inaongezeka siku baada ya siku. 864662
captcha