Amesema kuwa jambo muhimu zaidi katika wakfu ni kuchunga amana katika suala hilo.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa maudhui ya wakfu ni pana mno na kuongeza kuwa, kwa sasa kuna nyanja nyingi kwa ajili ya wakfu ikiwa ni pamoja na medani za tiba, elimu, uhakiki na utafiti, sayansi za kisasa, mazingira na kueneza dini kwa njia za kisasa.
Ayatullah Ali Khamenei amesisitiza juu ya umuhimu na udharura wa viongozi na wakurugenzi kusimamia vyema taasisi za wakfu na kusema kuwa usimamizi huo una maana ya kutekeleza majukumu kwa njia sahihi na kamili katika maudhui muhimu sana ya wakfu.
Amepongeza na kushukuru pia juhudi kubwa zilizofanywa na Hujjatul Islam Walmuslimin Muhammadi ambaye ni Mkuu wa Jumuiya ya Wakfu na Masuala ya Kheri hapa nchini, wakurugenzi na wafanyakazi wa taasisi hiyo. 971492