IQNA

Imam Ayatullah Khamenei:

Mapinduzi ya Kieneo yanapaswa kuainisha mipaka yake na ile ya ubeberu wa kimataifa

22:21 - December 11, 2012
Habari ID: 2462252
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Ali Khamenei amesema kuwa sharti kuu la kutekelezwa vyema mchango wa wahadhiri wa vyuo vikuu, wasomi na watu wenye vipawa kwa ajili ya harakati ya jamii kuelekea kwenye ufanisi na uokovu ni kuwa na ikhlasi, ushujaa, kuwa macho na kuchapakazi kwa bidii.
Ayatullah Khamenei ambaye mapema leo alikutana na mamia ya wahadhiri wa vyuo vikuu, wasomi na wanafikra wanaoshiriki katika mkutano wa kimataifa wa Wahadhiri wa Vyuo Vikuu na Mwamko wa Kiislamu hapa mjini Tehran ameweka wazi umuhimu wa mwamko wa Kiislamu na kusisitiza kuwa, wasomi, waandishi, washairi na hasa maulamaa wa kidini wana nafasi muhimu sana katika ufanisi na uokovu wa mataifa mbalimbali.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria woga wa maadui wanaposikia neno "mwamko wa Kiislamu" na kusema: Maadui wanafanya juhudi kubwa kuhakikisha kwamba neno mwamko wa Kiislamu halitumiwi kueleza harakati ya sasa katika eneo la Mashariki ya Kati kwa sababu maadui hao na woga na wasiwasi mkubwa kutokana na kuenea Uislamu halisi.
Ayatullahil Udhmaa Ali Khamenei amesema kuwa moja ya malengo ya mwamko wa Kiislamu ni kujiondoa katika shari ya udhibiti na ubeberu wa kimataifa. Amesema kuwa ni makosa kudhani kuwa ubeberu wa kimataifa unaoongozwa na Marekani yumkini ukaafikiana na harakati za Kiislamu kwa sababu Marekani itafanya kila iwezalo kuwaangamiza wanaharakati wa Kiislamu; hivyo basi mapinduzi yanayofanyika katika eneo hilo yanapaswa kuainisha mipaka yake na ubeberu wa kimataifa ili yasitumbike katika hadaa.
Ayatullah Khamenei amesema kuwa lengo jingine muhimu la mwamko wa Kiislamu ni kusimamisha Uislamu na sheria zake. Ameongeza kuwa zinafanyika njama kubwa za kutaka kuonesha kuwa sheria za Kiislamu hazioani na maendeleo, mageuzi na ustaarabu; ilhali Uislamu unatoa majibu ya mahitaji yote ya mwanadamu na umekuja kwa ajili ya karne na zama zote za maendeleo ya mwanadamu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, moja kati ya masuala muhimu katika mapinduzi ya wananchi wa Mashariki ya Kati ni kulinda uungaji mkono wa wananchi. Amesisitisza kuwa wananchi ndio wenye nguvu halisi na kila mahala ambapo wananchi wanawaunga mkono viongozi wao kwa umoja na mshikamano basi Marekani na wakubwa kuliko Marekani hawawezi kufuadafu.
Ayatullahil Udhmaa Khamenei ametilia mkazo udharura wa nchi za Kiislamu hususan zile zilizofanya mapinduzi kulea kizazi cha vijana kielimu na kiteknolojia kwa ajili ya kupata uwezo na kuongesza kuwa, jambo hilo linawezekana na kielelezo chake chenye mafanikio ni Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Vilevile amepongeza kazi ya wanamapambano wa Palestina katika vita vya hivi karibuni na utawala ghasibu wa Israel huko Gaza na kusema, hakuna mtu aliyekuwa akiamini kwamba katika vita vya Wapalestina na Israel Wapalestina wanaweza kuiwekea masharti Israel kwa ajili ya kusitisha mapigano.
Ameshiria pia machafuko ya Syria na kusema kuwa makundi ya waasi ndiyo sababu ya kuendelea mgogoro nchini humo. Amesisitiza kuwa matakwa yote ya Waislamu yanapaswa kukukidhiwa bila la kutumia mabavu.1152054


captcha