IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Kusimama kidete Iraq kumedhamini usalama wa eneo

22:50 - June 17, 2015
Habari ID: 3315772
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kusimama kidete taifa na serikali ya Iraq mbele ya magaidi na Matakfiri ni chanzo cha kudhamini usalama wa eneo la Mashariki ya Kati.

Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameyasema hayo leo Jumatano mjini Tehran wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Iraq Haidar al Abadi. Kiongozi Muadhamu ameongeza kuwa moja ya sifa kuu za watu wa Iraq iliyobainika katika vita dhidi ya ugaidi ni ushujaa, azma na uwezo wa vikosi vya kujitolea vya wananchi katika kukabiliana na adui. Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuchukua tahadhari ili kulinda umoja wa kisiasa na kitaifa Iraq ni jambo la dharura. Akiashiria azma, hima na ushujaa wa vijana Wairaqi katika vita dhidi ya magaidi, Kiongozi Muadhamu amesisitiza kuwa kuwa: "Uwezo mkubwa wa vikosi vya kujitolea vya wananchi ni jambo litakalokuwa na athari muhimu katika ustawi wa nyanja mbalimbali Iraq katika siku za usoni. Amebainisha kuwa, uwepo wa magaidi huko Iraq ni tukio la kupita na kwamba vikosi vya kujitolea vya wananchi vinapaswa kutumiwa pia katika medani zisizo za kivita. Ayatullah Khamenei amesema kuvuruga nguzo za umoja wa kitaifa na kisiasa nchini Iraq ni moja ya malengo ya mashirika ya kijasusi ya nchi za Magharibi nchini Iraq. Amesisitiza kuwa, kunapaswa kuchukuliwa tahadhari kamili katika kikabiliana na njama za kuibua mifarakano sambamba na kulinda umoja wa Mashia, Masuni, Wakurdi na Waarabu nchini Iraq. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kutoa uungaji mkono wa pande zote kwa serikali ya kisheria ya Iraq.
Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Iraq amebainisha furaha yake kukutana na Kiongozi Muadhamu na kusema himaya ya Iran kwa Iraq ni ishara ya kina cha uhusiano mzuri wa nchi mbili. Amesema magaidi wa Kitakfiri Iraq na Syria hawatafautishi baina ya Shia na Suni na kuongeza kuwa, Iraq imeweza kuzuia kuenea magaidi wa Daesh katika eneo la Mashariki ya Kati. Hata hivyo amesema nchi za eneo hilo zinapaswa kuungana ili kuangamiza kund hilo la kigaidi. Aidha ameishukuru kwa dhati Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa msaada wake kwa serikali na watu wa Iraq katika vita vyao dhidi ya ugaidi.../mh

3315760

captcha