IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Ni marufuku kufanya mazungumzo na Marekani

6:10 - October 08, 2015
Habari ID: 3383038
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa Marekani inasaka fursa ya kupenya na kulazimisha matakwa yake kwa taifa la Iran.

Ayatullah Ali Khamenei ambaye ni Amir Jeshi Mkuu wa majeshi yote ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo Jumatano mjini Tehran  katika hadhara ya makamanda na wafanyakazi wa kikosi cha majini cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah). Ameashiria  nafasi na mchango wa jeshi hilo katika kulinda usalama wa Iran na kusema:  Maadui wanataka kubadilisha mahesabu ya maafisa wa Iran na kubadili fikra za wananchi hususan vijana hivyo wananchi wote wanapaswa kuwa macho na makini.

Ameshiria upinzani wa taifa la Iran dhidi ya kufanya mazungumzo na Marekani na akasema: Ni marufuku kufanya mazungumzo na Marekani kwa sababu ya madhara yake mengi na jambo hilo halina maslahi kwa sababu Wamarekani wanafanya jitihada za kufungua njia ya kuwa na satua nchini Iran kupitia njia ya mazungumzo lakini Iran imekuwa macho kikamilifu kuhusu maudhui hiyo.

Amiri Jeshi Mkuu amesema, Iran kamwe haitakuwa ya kwanza kuanzisha vita na kuongeza kuwa: Uvamizi na kutaka kuwa na satua ni ada na tabia ya adui, kwa msingi huo kuna ulazima wa kuzidisha uwezo wa kielimu na zana kupitia uvumbuzi na ubunifu.

Ameashiria mipango hatari ya madola ya kibeberu kwa ajili ya eneo la Mashariki ya Kati na kusema: Madola hayo hayasiti kutumia silaha hatari sana na mbinu za kinyama kwa ajili ya kuua wanadamu wasio na hatia; na madai yao ya kutetea haki za binadamu na haki za raia ni kinyume na ukweli na hayana ukweli kabisa.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa mashambulizi yaliyofanywa dhidi ya hospitali nchini Afghanistan na mauaji ya wananchi katika nchi za Syria, Iraq, Yemen, Palestina na Bahrain ni mfano wa jinai zinazofanywa na madola ya kibeberu duniani. Ameongeza kuwa, Hii leo hatari kubwa zaidi kwa dunia ni unafiki, ria na urongo wa wale wanaodai kutetea haki za binadamu.

Ayatullah Khamenei ameashiria nafasi ya Iran katika kuzuia utekelezwaji wa njama za maadui na kusema: Kufeli kwa adui ndani na nje ya kanda hii kumetokana na baraka za kuwa macho, utayarifu na nguvu za Jamhuri ya Kiislamu na kwa msingi huo uadui mkubwa zaidi wa madola ya kibeberu unaelekezwa kwa Iran na suala la kufanyika mazungumzo pia limeibuliwa katika fremu ya siasa za madola ya kibeberu kwa ajili ya kupenya na kuingia Iran.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa Iran haipingi asili ya kufanya mazungumzo na nchi mbalimbali zikiwemo za Ulaya na zisizo za Ulaya na kuongeza kuwa, lakini suala hilo ni tofauti kuhusu Wamarekani kwa sababu kufanya mazungumzo na Iran katika mtazamo wao kuna maana ya kufungua njia kwa ajili ya kupenya katika nyanja mbalimbali za kiuchumi, kiutamaduni, kisiasa na kiusalama hapa nchini.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa hii leo pia taifa la Iran litamuondoa adui katika medani kutokana na nguvu yake ya kimaanawi na wale wanaoutakia mabaya mfumo wa Kiislamu watashindwa katika mipango na njama zao za kiusalama, kijeshi, kiuchumi na kiutamaduni...

3382718

captcha