IQNA

Kiongozi Muadhamu katika mkutano na waziri mkuu wa Ugiriki

Nchi za Ulaya ziwe na misimamo huru mbele ya Marekani

7:16 - February 09, 2016
Habari ID: 3470124
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Ayatullah Ali Khamenei, amesema kuwa, nchi za Ulaya zina haki ya kukosolewa na kwamba tofauti na huko nyuma hivi sasa nchi za bara hilo hazina misimamo huru mbele ya Marekani, na watu wa Ulaya wana wajibu wa kuondoa udhaifu wao huo.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyasema hayo Jumatatu mjini Tehran alipokutana na Alexis Tsipras, Waziri Mkuu wa Ugiriki na kusisitiza kuwa, hivi sasa Ulaya inatakiwa kurekebisha udhaifu wake huo mbele ya Marekani. Akiashiria historia inayong'ara ya kunawiri uhusiano wa kiutamaduni na kiustaarabu baina ya Iran na Ugiriki, Ayatullah Khamenei amesema kuwa, safari ya waziri mkuu huyo wa Ugiriki hapa nchini inaweza kuwa mwanzo mzuri kwa ajili ya kuongeza mabadilishano na ushirikiano ya muda mrefu baina ya nchi mbili. Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria maneno ya Tsipras kuhusiana na kadhia ya Syria na kusema kuwa, ugaidi ni ugonjwa hatari sana wa kuambukiza ambao ikiwa kila upande utachukua hatua za kweli za kukabiliana nao, basi unaweza kutokomezwa. Hata hivyo amesema, kwa bahati mbaya baadhi ya pande zinayaunga mkono makundi ya kigaidi kwa njia ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja. Akiashiria piaya nukta za ushirikiano na kuwa na misimamo sawa baina ya Iran na Ugiriki, Ayatullah Khamenei amesema kuwa, serikali ya Athens ina siasa na sera za kujitegemea na kuongeza kuwa, anataraji kuona nchi hiyo inayashinda matatizo yake ya kiuchumi na kusisitiza kuwa ujumbe wa Ugiriki uliokuja hapa Tehran utaandaa mazingira ya kulindwa vizuri maslahi ya pande mbili. Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Ugiriki, Alexis Tsipras, amemshukuru Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mchango wake mkubwa katika masuala mbalimbali na sambamba na kusema kuwa, Iran ni taifa kubwa amesisitiza kuwa safari yake hapa nchini ni ishara ya kuwepo irada ya kisiasa ya pamoja kwa ajili ya kuongeza ushirikiano katika ngazi zote baina ya Iran na Ugiriki.

3474074

captcha