IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi asisitizia kulindwa mazingira mazingira ya kijani kibichi

20:12 - March 08, 2016
Habari ID: 3470187
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo amepanda mche mmoja wa mti katika Wiki ya Maliasili nchini Iran na kusisitiza kuhusu kulindwa mazingira.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu baada ya kupanda mche huo amesisitiza udharura wa kujua mimea na miti ambayo ni chimbuko la baraka katika maisha ya mwanadamu. Amesema wananchi na maafisa wa serikali wanapaswa kuzingatia suala la kulinda mazingira ya kijani kibichi hasa misitu.

Ameashiria kuharibiwa mimea asili na ya kienyeji kutokana na usimamizi mbovu wa baadhi ya wanaosimamia misitu na kusema: "Kuhujumiwa misitu na mabustani ni kinyume na maslahi kutokana na kuwa baadhi ya spishi asili za mimea huharibiwa. Kwa msingi huo kulinda mazingira ya kijani kibichi ni jukumu la wote."

Wengine waliohudhuria hafla hiyo ya kupanda mche ni Waziri wa Jihadi ya Kilimo na Meya wa jiji la Tehran.

3481841

captcha