IQNA

Wapalestina waandamana Ghaza kulaani mzingiro wa Utawala wa Kizayuni

18:46 - May 09, 2016
Habari ID: 3470303
Mamia ya Wapalestina wameandamana katika Ukanda wa Ghaza kulaani mzingiro wa kibaguzi wa takriban mwongo mmoja uliowekwa na Utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya eneo hilo.

Waandamanaji hao walikuwa wamebeba picha za watoto watatu waliopoteza maisha jana baada ya nyumba yao kuteketea katika kambi ya wakimbizi ya al-Shati katika Ukanda wa Ghaza. Mkasa huo wa moto uliripotiwa kusababishwa na mshumaa kutokana na kuwa umeme umekuwa ukikatika mara kwa mara katika ukanda huo.

Hii ni katika hali ambayo, askari wa Utawala haramu wa Israel wameanzisha chokochoko mpya dhidi ya Wapalestina wa Ghaza. Siku ya Jumatano, askari wa Utawala haramu wa Kizayuni walishambulia maeneo ya mpakani mwa Ukanda wa Ghaza ambapo katika kujibu hujuma hiyo, wanamuqawama wa Palestina walipambana na askari hao.

Mashambulio yanayoendelea kufanywa na jeshi la utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza ni ukiukaji wa makubaliano ya usitishaji vita yaliyofikiwa baina ya pande mbili mwezi Agosti mwaka 2014 baada ya vita vya siku 50, ambapo Utawala haramu wa Israel uliwaua shahidi zaidi ya Wapalestina 2,300 wakiwemo wanawake na watoto na kuwajeruhi maelfu ya wengine.

Baada ya kupita miaka 10, eneo la Ukanda wa Ghaza, Palestina inayokaliwa kwa mabavu lingali limewekewa mzingiro na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel kwa ushirikiano wa Misri; na kutokana na kuendelea kukumbwa na mashambulio ya ndege za utawala huo ghasibu, fursa la kulikarabati na kulijenga upya eneo hilo imebaki kuwa ndoto.

Hali ngumu na ya kusikitisha waliyonayo wakazi wa Gaza na magofu yaliyosalia kutokana na uharbifu uliosababishwa na moto wa vita uliowashwa na Israel vimeshatolewa tahadhari na indhari mara kadhaa na Umoja wa Mataifa.

/3459755

captcha