IQNA

Washindi wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Iran watangazwa

2:04 - May 18, 2016
1
Habari ID: 3470316
Jopo la majaji limewatangaza washindi katika Mashindano ya 33 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu mjini Tehran.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, katika kategoria ya qiraa, mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran , Qarii Hamed Walizadeh alichukua nafasi ya kwanza huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Mohammad Javid Akbari wa Afghanistan na Bahre Al Din Said wa Indonesia akishika nafasi ya tatu. Sayed Abbas Ali wa Ujerumani na Mustafa Ali wa Uholanzi walishika nafasi za nne na tano kwa taratibu.

Katika kategoria ya kuhifadhi Qur’ani kikamilifu, nafasi ya kwanza hapa pia imeshikwa na mwakilishi wa Iran Mojtaba Fard Fani akifuatiwa na Abdul Aziz Ahmed wa Misri huku Muhammad Ali Abdullah wa Australia akishika nafasi ya tatu kwa taratibu.

Khalid Sankari wa Kodivaa na Muhammad Taha Hassan wa Niger wamechukua nafasi za nne na tano kwa taratibu.

Mashindano ya 33 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yalizinduliwa rasmi Jumatano iliyopita katika Ukumbi Mkubwa wa Sala wa Imam Khomeini MA mjini Tehran.

Nchi zaidi ya 70 zilituma wawakilishi katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ambayo yalikuwa na washiriki 130. Kaulimbiu ya mashindano ya mwaka huu ilikuwa ni "Kitabu Kimoja Umma Moja”.


3499106



Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Micky Msekwa
0
0
Mashaallah washiriki woote katika shindano hili ALLAH awazidishie elimu na fahamu na hifadhi zaidi na zaidi, na awajaalie kupitia kuhifadhi na kusoma kwenu QUR'AN malipo makubwa na awajaalie nyie pamoja na tuyafate yale yaliomo katika QUR'AN na kuyaacha alio yakataza.... AMIIN....

Nataka kujua listi ya Majina 10 ya walio shinda na nchi walizotoka wa kwanza mpaka wa kumi in shaa allah.....
captcha