IQNA

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani yazinduliwa Tehran

17:06 - June 14, 2016
Habari ID: 3470385
Waziri wa Utamaduni na Muongozi wa Kiislamu Iran Ali Jannati amefungua Maoneysho ya 24 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu mjini Tehran Jumatatu usiku.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, ufunguzi wa maoneysho hayo umehudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu akiwemo Naibu Waziri Utamaduni na Muongozi wa Kiislamu Iran anayesimamia masual ya Qur'ani Sheikh Mohammad Ridha Heshmati, Mkuu wa Shirika la Hija la Iran Saeed Ouhadi pamoja na wanazuoni na maustadh wa Qur'ani Tukufu.

Kikao hicho kilianza na qiraa ya Qur'ani Tukufu ya qarii mashuhuri Muirani Ustadh Mohammad Hussein Saeedian.

Sheikh Heshmati amesema maonyesho ya Qur'ani ni fursa ya wanaharakati wa Qur'ani kukutana na kutumia uwezo wao ili watu waweze kuifahamu Qur'ani zaidi.

Amesema kaulimbiu ya maonyesho ya mwaka huu ni "Kuelekea Katika Ufahamu wa Qur'ani."

Kwa upande wake Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu ameashiria hadhi ya juu ya Qur'ani Tukufu kama kitabu cha kumuongoza mwanadamu na kusema, pengo kubwa zaidi katika jamii ya Waislamu ni kuipuuza Qur'ani na mafundisho yake katika maisha.

Maonyesho ya mwaka huu, ambayo yatamalizika 30 Juni, yatakuwa na vibanda 300 huku kitengo cha vitabu kikiwa kikubwa zaidi.

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tehran ni makubwa zaidi ya aina yake duniani.

Maonyesho hayo hufanyika kila mwaka katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Tehran ambapo huwa na vitengo kadhaa vya maudhui mbali mbali za Qur'ani.

3460082

captcha