IQNA

Wananachi wa Iran waandamana kulaani jinai za koo Aal Saud na Aal Khalifa

12:43 - September 10, 2016
Habari ID: 3470556
Mamilioni ya wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wameandamana kote nchini kulaani jinai za tawala za kikoo za Aal Saud huko Saudi Arabia na Aal Khalifa huko Bahrain kwa jinai zao dhidi ya watu wa eneo.

Katika maandamano hayo ya Ijumaa, washiriki pia  wamelaani mauaji ya umati yaliyofanyika dhidi ya Mahujaji Wairani na wasiokuwa Wairani mikononi mwa utawala wa Aal Saud katika ibada ya Hija mwaka jana huko Mina. Aidha wamelaani vikali ukandamizaji wa kinyama unaofanywa na utawala wa Aal Khalifa dhidi ya watu wanaodhulumiwa wa Bahrain. Waandamanaji hao pia wamebainisha uungaji mkono wao kwa mwanazoni maarufu wa Bahrain Sheikh Issa Qassim anayedhalilishwa na utawala wa Aal Khalifa.

Wananchi wa Iran wamewakumbuka wale wote waliokufa shahidi katika maafa wa Mina  na kutaka kamati ya kutafuta ukweli iundwe ili kuchunguza maafa hayo sambamba na kupewa haki na fidia familia za mashahidi.

Katika taarifa iliyotolewa katika maandamano hayo, waandamanaji wameuonya utawala wa Aal Saud kuwa iwapo hautakubali dhima ya maafa ya Mina na iwapo hautaacha uchochezi katika nchi za Kiislamu, na iwapo utawala wa Aal Khalifa hautaacha kuwakandamiza wananchi madhulumu wa Bahrain na kuwavunjia heshima wanazuoni wa kidini hasa Sheikh Issa Qassim, basi tawala hizo mbili zisubiri ghadhabu ya kimapinduzi ya vijana wa nchi za Kiislamu.

Wakati huo huo mkuu wa Shirika la Hija la Iran amesema Saudi Arabia imewazuia Wairani kuhiji mwaka huu sambamba na kukataa kujadili njia za kuzuia kujirudia tena maafa kama yale yaliyojiri Mina. Saeed Ohadi amesema ni jambo lisilokubalika kwa Saudia kuwauzia Wairani kuhiji hasa kwa kuzingatia kuwa kuna watu ambao wako katika orodha ya kusubiri Kuhiji miaka 15 hadi 20 ijayo. Ameongeza kuwa, Saudia inaamini kuwa miji mitakatifu ya Makka na Madina ni milki yake katika hali ambayo maeneo hayo matakatifu ni milki ya Waislamu wote.

3529102Wananachi wa Iran waandamana kulaani jinai za koo Aal Saud na Aal Khalifa


Wananachi wa Iran waandamana kulaani jinai za koo Aal Saud na Aal Khalifa

Wananachi wa Iran waandamana kulaani jinai za koo Aal Saud na Aal Khalifa

Wananachi wa Iran waandamana kulaani jinai za koo Aal Saud na Aal Khalifa

Wananachi wa Iran waandamana kulaani jinai za koo Aal Saud na Aal Khalifa

captcha