IQNA

Nyaraka za Siri

Mahujaji 874 walifariki mwa huu katika Hija Saudi Arabia

13:35 - September 19, 2016
Habari ID: 3470571
Huku Saudi Arabia ikijaribu kudai kuwa Ibada ya Hija iliandaliwa kwa mafanikio mwakubwa mwaka huu bila tatizo lolote, ripoti iliyovuja inaonyehsa kuwa mahujaji zaidi ya 800 walifariki wakati wa Hija.

Kwa mujibu wa nyaraka zilizofiichuka kutoka Wizara ya Afya ya Saudia, mahujaji 874 walipoteza maisha katika msimu wa Hija mwaka huu kutokana na sababu mbali mbalai.

Hii ni katika hali ambayo idadi jumla ya Mahujaji mwaka huu ilikuwa ndogo sana ikilinganishwa na mwaka jana.

Aghalabu ya waliofariki dunia katika ibada ya Hija mwaka huu walikuwa ni watu 239 kutoka Saudi Arabia, huku Misri, Pakistan, Bangladesh, Nigeria, Indonesia na India zikipoteza mahujaji 51, 84,43,31,124 na 64 kwa taratibu.

Karibu Waislamu milioni 1.5 walitekeleza Ibada ya Hija katika mji mtakatifu wa Makka wiki iliyopita.

Mwaka jana mahujaji zaidi ya 7000 walipoteza maisha katika Ibada ya Hija eneo la Mina karibu na Makka mwaka jana. Tukio hilo lilijiri siku chache baada ya mahujaji zaidi ya 100 kupoteza maisha kufuatia kuanguka winchi au kreni katika Msikiti Mtakatifu wa Makka karibu na Kaaba Tukufu.

Watawala wa Saudia wanaluamiwa kwa usimamizi mbovu wa Ibada ya Hija jambo ambalo limepelekea idadi kubwa ya mahujaji kupoteza maisha kila mwaka.


3460967
Kishikizo: hija mina saudi arabia iqna
captcha