IQNA

Hafla ya kupandisha bendera ya Imam Hussein AS katika Msikiti wa Ghadir, Dar+ Video, Picha

14:39 - October 08, 2016
Habari ID: 3470604
Hawza Imam Swadiq (a.s) na Masjid al Ghadiir katika mji wa Dar es Salaam Tanzania imeshuhudia tukio la kupandishwa Bendera ya Imam Hussein AS.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Hawza (Chuo Kikuu cha Theolojia ya Kiislamu) hiyo inayoongozwa na Maulana Sheikh Hemedi Jalala imesimamia tukio la kupandishwa bendera ya Imam Hussein Masjid Al Ghadiir mapema alasiri tarehe 5 Oktoba.

Taarifa iliyotolewa na chuo hicho imesema malengo ya bendera hiyo ni kuonyesha ishara ya kuitikia wito wa Imam Hussein AS na kutoa kiapo kwa Imam wa zama, Imam Mahdi (Mwenyezi Mungu Aharakishe Kudhihiri Kwake)

Hafla hiyo ilisimamiwa na Sheikh Muhammad Abdi naibu mkuu wa Sheikh Jalala alisimamia tukio ambaye alibainisha kuhusu falsafa na mantiki ya kupandisha bendera hiyo. Waislamu wa matabaka mbali mbali walihudhuria hafla hiyo.

Alisema bendera hii ni ishara ya kukataa udhalili, udhalili kwa mtu binafsi, kwa mnyonge yeyote na kwa kila anaeonewa katika mgongo wa ardhi, kuapandisha bendera hii ni kuitikia wito wa Imam Hussein wa kuwanusuru wanyonge na kuilea jamii nzima bila kubagua dini zao wala rangi zao.

Akizungumza na mwandishi wa IQNA, Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Tanzania Ali Bagheri amesema mbali na upandishaji wa bendera hiyo amesema aghalabu ya washiriki katika hafla hiyo ni Mashia wa kizazi kipya na kizazi cha kwanza nchini Tanzania.

Amesema mafundisho ya Imam Hussein AS yameleta mabadiliko makubwa katika jamii ambapo hivi sasa kuna idadi kubwa ya vijana wanaowapenda Ahul Bayt AH na wanaouamini mfumo wa Utawala wa Faqihi.

Bendera hiyo imepandishwa katika siku hizi za kwanza za 10 za Mwezi wa Muharram ambapo Waislamu na wapenda haki kote duniani wanakumbuka  tukio la Ashura, miaka 1377 iliyopita kulingana na kalenda ya Hijria Qamaria.

Katika tukio hilo, moja kati ya vita mashuhuri katika historia ya Kiislamu na ya mwanadamu, vilitokea baina ya majeshi ya haki na batili katika ardhi ya Karbala huko Iraq. Siku hii inajulikana kwa jina la Ashura. Katika siku hiyo mjukuu wa Mtume SAW, Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib AS, alisimama kishujaa na wafuasi wake waaminifu 72, kukabiliana na jeshi la batili ili kuilinda dini ya Allah. Hamasa ya Karbala ilikuwa dhihirisho la mambo mawili makuu. Kwanza ni ujasiri, ushujaa, moyo wa kujitolea, uaminifu pamoja na kuyapokea kwa moyo mkunjufu mauti ya kuuawa shahidi, sifa walizojipamba nazo wapiganaji wachache wa jeshi la haki wakiongozwa na Imam Hussein AS dhidi ya Yazid bin Muawiya.

Pili ni upeo wa ukatili, udhalimu na unyama ulioonyeshwa na jeshi batili la Yazid bin Muawiya. Baada ya kupambana kishujaa, hatimaye mjukuu huyo wa Mtume Muhammad SAW aliuawa shahidi katika siku hiyo ya Ashura.



Hafla ya kupandisha bendera ya Imam Hussein AS katika Msikiti wa Ghadir, Dar+ Video, Picha



Hafla ya kupandisha bendera ya Imam Hussein AS katika Msikiti wa Ghadir, Dar

Hafla ya kupandisha bendera ya Imam Hussein AS katika Msikiti wa Ghadir, Dar


Hafla ya kupandisha bendera ya Imam Hussein AS katika Msikiti wa Ghadir, Dar

3536304


Hafla ya kupandisha bendera ya Imam Hussein AS katika Msikiti wa Ghadir



captcha