IQNA

Uislamu ni dini inayoenea kwa kasi zaidi Ireland

22:19 - October 28, 2016
Habari ID: 3470640
IQNA-Uislamu ni dini inayoenea kwa kasi zaidi nchini Ireland huku kukiimarishwa jitihada za kuelimisha jamii kuhusu Uislamu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kuna Waislamu zaidi ya 50,000 wanaoishi nchini Ireland lakini pamoja na hayo, kuna ripoti za chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu nchini humo.

Ili kukabiliana na hali hiyo, Waislamu Ireland wametakwa kuwasilisha malalamiko yao kila wakati vyombo vya habari vinavyoeneza habari zisizo sahihi kuhusu Uislamu.

Bi. Raneem Salah amesema ameishi vizuri nchini Ireland kwa muda wa miaka sita lakini anasema kuna Waislamu wenzake ambao wamepata matatizo kwa ajili ya dini yao na hasa wanawake wamekuwa wakisumbuliwa kutokana na kuvaa Hijabu.

Raneem ambaye ni mwanafunzi wa taaluma ya tiba katika Chuo Kikuu cha Dublin, UCD, anasema ubaguzi unaenea zaidi kutokana na kuwa hakuna Waislamu katika vyombo vya habari. Anaongeza kuwa: "Nadhani kuna umuhimu wa kuhakikisha kuwa tuna watu ambao wanaeneza ujumbe sahihi kuhusu Uislamu kwani wengi hawawawajui Waislamu na wala wahajui lolote kuhusu Uislamu." Anasema la kusikitisha ni kuwa wengu wanaunasibisha Uislamu na ugaidi.

Kwa mujibu wa takwimu za idadi ya watu za mwaka 2011, kuna Waislamu 50,000 wanaoishi Ireland, hii ikiwa ni mara mbili zaidi ya Wakristo wa pote la Presbyterian nchini humo.

3461252

captcha