Kwa mujibu
wa uchunguzi wa maoni, asilimia 31 ya Waislamu Uingereza wanaamini kuwa
serikali ya Marekani ilihusika moja kwa moja katika hujuma
zilizotekelezwa
dhidi ya majengo pacha ya Kituo cha Biashara Duniani mjini New York na
dhidi ya jengo la Pentagon mjini Washington. Uchunguzi huo wa taasisi
ya Policy Exchange umebaini kuwa ni
asilimia nne tu ya Waislamu Uingereza wanaoamini taarifa rasmi kuwa kundi la Al
Qaeda ndilo lililotekekeza hujuma hiyo ya kigaidi ya Septemba 11, 2001.
Halikadhalika asilimia 7 ya Waislamu Uingereza wanaamini kuwa hujuma hizo za
kigaidia zilitekelezwa na Wazayuni (Mayahudi) na wala si Al Qaeda. Uchunguzi huo
uliowahusisha Waislamu 3,000 unaoneysha kuwa asilimia 52 wanasema hadi sasa
hawawezi kubaini kwa hakika ni nani aliyetekeleza hujuma hiyo ya kigaidi. Itakumbukwa kuwa baada ya hujuma za 9/11 kulishuhudiwa wimbi kubwa la chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu katika nchi za Magharibi.
Kwingineko, uchunguzi huo wa maoni umebaini kuwa asilimia 71 ya Waingereza wasiokuwa Waislamu wanaamini kundi la Al Qaeda ndilo lililotekeleza hujuma hiyo huku asilimia 10 wakiamini ni Rais wa wakati huo wa Marekani, George W Bush ndie aliyetekeleza hujuma hiyo na wengine asilimia moja wakisema ugaidi huo ulitekelezwa na Wazayuni.
Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2011, idadi ya Waislamu Uingereza ni takribani Milioni tatu au asilimia 5 ya wakaazi wa nchi hiyo ya Ulaya Magharibi.