IQNA

Bunge la Misri latakiwa kuongeza bajeti ya mashindano ya Qurani

13:20 - May 17, 2017
Habari ID: 3470983
TEHRAN (IQNA) Wizara ya Waqfu na Masuala ya Kidini Misri limetoa wito wa kuongezwa bajeti ya mashindano ya Qur'ani nchini humo.

Taarifa zinasema katika kamati ya bajeti katika Bunge la Misri imekutana na wawakilishi wa Wizar ya Waqfu na kutoa wito wa kuongezwa bajeti ya mashindano ya Qur'ani.

Katika kikao hicho, mashindano ya Qur'ani yametajwa kuwa yenye umuhimu mkubwa na kwa msingi huo kuna haja ya kuongeza bajeti ili kuyaimarisha.

Aidha washiriki katika kikao hicho wametaka serikali itenge bajeti zaidi kwa ajili ya kusimamisi misikiti nchini humo.

Misri ni nchi ya Waislamu iliyo Afrika Kaskazini na usomaji Qur'ani nchini humo ni mashuhuri sana. Aidha Misri inatambulika kama nchi yenye wasomi bora zaidi wa Qur'ani duniani. Miongoni mwa maqarii mashuhuri wa Qur'ani Tukufu nchini Misri ni pamoja na Maustadh Abdul Basit Abdus Samad, Mohammed Siddiq Al-Minshawi, Shahat Mohamed Anwar, and Mustafa Esmail.

3599980

Kishikizo: qurani misri
captcha