IQNA

Waislamu Myanmar wazuiwa kushiriki katika Ibada ya Hija

14:07 - August 10, 2017
Habari ID: 3471117
TEHRAN (IQNA)-Mabuddha nchini Myanmar wamewazuia Waislamu 21 wa kabila la Rohingya kutekeleza ibada ya Hija mwaka huu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Waislamu 21 wa kabila linalokandamizwa la Rohingya kutekeleza ibada ya faradhi ya Hija. Taarifa zinasema Mabuddha wenye misimamo mikali waliwazuia Mahujaji kutoka mji wa Akyab (Sittwe) ambao ni mji mkuu wa jimbo la Waislamu la Rakhine kuondoka kwa ajili ya kutekelaza Ibada ya Hija. Taarifa zinasema pamoja na kuwa Waislamu hao walikuwa na kibali cha wizara ya masuala ya kidini ya Myanmar kutekeleza ibada ya Hija, lakini Mabuddha wenye misimamo mikali walizingira msafara wao na kuwazuia kuendelea na safari.

Walioshuhudia wanasema maafisa wa usalama walipofika eneo hilo walipuuza kibali hicho na wakawaamuru Waislamu hao warejee makwao.

Tangu muongo wa 1960 serikali ya Myanmar ilianzisha mikakati kabambe ya kuwabinya na kuwashinikiza Waislamu wa jamii ya Rohingya ya nchi hiyo ili waache mashamba, nyumba na milki zao na kuondoka nchini humo. Mwaka 2012 serikali ya Myanmar ilizidisha mashinikizo ya kisiasa na kuchochea mashambulizi na mauaji ya Mabudha wenye misimamo mikali dhidi ya Waislamu hao.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa Waislamu wa kabila la Rohingya ni jamii ya wachache duniani inayodhulumiwa na kunyongeshwa zaidi. Serikali ya Myanmar inakataa kuwapa haki za uraia Waislamu hao ambao idadi yao ni zaidi ya watu milioni moja na laki tatu.

Katika miaka ya karibuni, Waislamu wengi wa kabila la Rohingya nchini Myamnar wameuawa au kulazimika kuhama makazi yao na kuwa wakimbizi katika nchi za Thailand, Malaysia na Indonesia kutokana na mashambulio ya Mabudha wenye misimamo ya kufurutu mpaka wanaoungwa mkono na serikali ya nchi hiyo.

3628896

captcha