IQNA

Muindonesia mwenye umri wa miaka 104 safarini Hija+PICHA

15:28 - August 27, 2017
Habari ID: 3471144
TEHRAN (IQNA)-Bi. Baiq Mariah kutoka Indonesia ametmabuliwa kuwa Hujaji mwenye umri wa juu zaidi mwaka huu.

Mariah, mwenye umri wa miaka 104 aliwasili Jumamosi mjini Jeddah Saudi Arabia na kupokelewa na afisa wa ubalozi wa Indonesia mjini humo na maafisa kadhaa wa Saudia.

Amesema safari yake hii ya kwanza ya Hija mwaka huu ni ndoto aliyokuwa nayo kwa muda mrefu. Walioandamana naya wanasema Bi Mariah aliwasili Saudia akiwa katika afya nzuri na atakuwa na uwezo wa kutekeleza Ibada ya Hija pasina kuwepo matatizo, Inshallah. Bi. Mariah ni miongoni mwa Mahujaji 221,000 kutoka Indonesia wanaotekeleza Ibada ya Hija mwaka huu.

Aghalabu ya Mahujaji kutoka Indonesia ni wazee na hilo hupelekea kuwepo changamoto za kiafya. Mwaka huu Waindonesia 20 hadi sasa wameshaaga dunia wakiwa katika Ibada ya Hija.

Hivi sasa kuna Waindonesia milioni 1 ambao wameorodhesha majina yao wakisubiri kupata fursa ya kutekeleza Ibada ya Hija na wengi, kwa wastani, husubiri miaka sita kabla ya zamu yao kuwadia. Saudi Arabia hutenga idadi maalumu ya mahujaji kutoka kutoka kila nchi na hivyo idadi hiyo haiwezi kuzidishwa. Kwa kawaida idadi ya Mahujji huenda na idadi ya Waislamu katika nchi husika na kwa msingi huo nchi zenye idadi kubwa ya Waislamu hutengewa nafasi nyingi za mahujaji.

Muindonesia mwenye umri wa miaka 104 safarini Hija+PICHA


Muindonesia mwenye umri wa miaka 104 safarini Hija+PICHA




3634782
captcha