IQNA

9:51 - September 24, 2017
News ID: 3471189
TEHRAN (IQNA) Jumuiya ya Kiislamu ya Maelewano ya Kitaifa ya Bahrain (Al Wefaq) imelaani hatua ya vikosi vya usalama kuhujumu madhihirisho ya Ashura na kuendelea kuzingirwa nyumba ya mwanazuoni wa Kiislamu Sheikh Issa Qassim.

Uhuru wa kuandaa hafla za kidini na kimadhehebu ni kati ya haki za kimsingi za mwanadamu lakini pamoja na kuwepo indhari kutoka mashirika ya kitaifa na kimatiafa ya kutetea haki za binadamu kuhusu haki hii, utawala wa Aal Khalifa nchini Bahrain ungali unaendelea kukiuka haki za Waislamu nchini Bahrain.

Duru za kisiasa Bahrain zinasisitiza kuwa hatua za utawala wa Aal Khalifa kuhujumu madhihirisho ya maombolezo ya mwezi wa Muharram ni mbinu iliyofeli katika miaka ya nyuma. Kwa hakika utawala wa Aal Khalifa nchini Bahrain kwa kuhujumu nembo zozote za maombolezo ya kuuawa shahidi Imam Hussein AS katika mwezi wa Muharram, unalenga kuoneysha kuwa mgogoro wa sasa wa Bahrain umeibuliwa na kundi la watu wa madhehebu moja.

Utawala wa Bahrain kwa hatua zake kama hizo cha kichochezi, unalenga kuvuruga ibada na mijimuiko ya kidini na kuifanya kuwa tishio la usalama ili kuedeleza siasa zake potovuza kuigawa vipande vipande jamii ya nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi.Lakini muelekeo kama huo wa utawala wa Aal Khalifa utazidi tu kufichua kashfa ya utawala huo na kubainisha utambulisho wake wa kuibua mifarakano katika jamii. Lengo kuula utwala wa Aal Khalifa katika kukabiliana na nembo za Kiislamu ni kuwapokonya Wabahrain uhuru wa kidini na kimadhehebu. Matukio ya hivi karibuni Bahrain yanaashiria kushadidi ukandamizaji wa utawala wa wapinzani huku idadi kubwa ya wanaharakati wakitiwa mbaroni. Aidha sambamba na hilo Waislamu wa madhehebu ya Shia, ambao ndio wengi Bahrain, wamewekewa vizingiti vingi sana katika kutekeleza ibada na hafla zao za kidini. Kila mwaka, wakati wa kuwadia Mwezi wa Muharram, wanajeshi wa utawala wa kiimla wa Aal Khalifa huvamia mitaa mbali mbali na kukusanya nembo zote, hasa mabango ambayo hutumika katika maombilezo ya Imam Hussein AS, imamu wa tatu wa Waislamu wa madhehebu ya Shia.Ufalme wa kiimla Bahrain walaaniwa kwa kukandamiza maombolezo ya Muharram

Utawala wa Aal Khalifa, mbali na kuvunjia heshima matukufu wa Kiislamu ya watu wa Bahrain na kuchana nembo zote za maombolezo tukio la Ashura, pia huvamia na kubomoa Husseiniya (kumbi za kidini za Mashia) na misikiti.

Utawala wa Aal Kahlifa unaendeleza udikteta wake kwa kukiuka haki zote za watu wa Bahrain. Utawala huo wa ukoo wa Aal Khalifa unalenga kuhujumu itikadi za Kiislamu za Wabahrain ili kuwalazimu wananchi wakubali sera za ubabe za ukoo huo dhalimu. Ukiukwaji haki za watu wa Bahrain haishii tu katika kupiga marufuku vyam vya kisiasa na kuwahukumu vifungo vya jela wanazuoni wa Kiislamu na viongozi wa watu wa Bahrain bali utawala wa Aal Khalifa unahujumu pia itikadi za kidini ikiwa ni pamoja na majlisi za kumuomboleza Imam Hussen AS na kukumbuka tukio chungu la Ashura katika Mwezi wa Muharram katika maeneo mbali mbali ya Bahrain.

Utawala uliopo Bahrain hivi sasa unatumia mbinu kadhaa kuzima mwamko wa watu wa Bahrain na kuwaondoa wapinzani katika medani za kijamii na kisiasa na ndio sababu ya kushuhudiwa kukamatwa na kufungwa kiholela wapinzani huku wengine wakiwekwa katika vifungo vya nyumbani. Matukio ya sasa ya Bahrain yanaonyesha kwa utawala wa Aal Khalifa na uwasi wasi mkubwa kuhusu irada na itikadi za kidini za wananchi kwani ni itikadi hizo ndizo zinachoimarisha mwamko na mori wa kutaka kupambana na udikteta. Sera kama hizo zimepelekea Wabahrain waendelee kuuchukia utawala wa Al Khalifa.Ufalme wa kiimla Bahrain walaaniwa kwa kukandamiza maombolezo ya Muharram

Itakumbukwekuwa miaka 1378 iliyopita kulingana na kalenda ya Hijria, moja kati ya vita mashuhuri katika historia ya Kiislamu na ya mwanadamu, vilitokea baina ya majeshi ya haki na batili katika ardhi ya Karbala huko Iraq. Siku hii inajulikana kwa jina la Ashura ambayo ni siku ya 10 ya Mwezi wa Muharram. Katika siku hiyo mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hussein AS, alisimama kishujaa na wafuasi wake waaminifu 72, kukabiliana na jeshi la batili la Yazid bin Muawiya ili kuilinda dini ya Allah.

3643984

Name:
Email:
* Comment: