IQNA

Msikiti wavunjiwa heshima Ujerumani

23:40 - October 27, 2017
Habari ID: 3471232
TEHRAN- (IQNA)-Watu wenye chuki dhidi ya Uislamu wameuvunjia heshima msikiti ambao bado unajengwa katika mji wa Frankfurt, Ujerumani Jumanne.
Msikiti wavunjiwa heshima UjerumaniTaarifa zinasema watu wasiojulikana wameweka kichwa cha nguruwe katika eneo la msikiti unaojengwa na Jumuiya ya Waislamu wa Uturuki ijulikanayo kama Ditib. Kumekuwepo na upinzani mkali wa ujenzi wa mji huo. Taarifa zinasema wakaazi wa mji huo wameandamana mara kadhaa kupinga ujenzi wa msikiti huo wakitaka leseni yake ibatilishwe.

Jumuiya ya Waislamu wa Uturuki inafadhili misikiti 900 kote Ujerumani, nchi ambayo ina Waislamu milioni tatu wenye asili ya Uturuki.

Katika miaka ya hivi karibuni kumeshuhudiwa ongezeko kubwa la chuki dhidi ya Waislamu huku chama cha AfD kinachopinga Waislamu kikipata asilimia 13 ya kura katika uchaguzi wa mwezi jana nchini humo.

3656999

captcha