IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Mapambano dhidi ya utawala haramu wa Israel yadumishwe

15:35 - November 01, 2017
Habari ID: 3471242
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma ujumbe katika Mkutano wa Pili Muungano wa Kimataifa wa Maulama wa Muqawama unaofanyika huko Lebanon akiagiza kudumishwa mapambano ya aina mbalimbali dhidi ya utawala vamizi na wa Kizayuni wa Israel kwa wale wote wanaohisi kubeba dhima na wajibu huo mkubwa.

Ayatullah Ali Khamenei amesema katika ujumbe huo uliokabidhiwa kwa Sheikh Maher Hammoud Mwenyekiti wa Muungano wa Kimataifa ya Maulama wa Muqawama kwamba: Jukumu zito na lisiloweza kusahaulika la Palestina liko kwenye mabega ya Umma wote wa Kiislamu. 

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Hapana shaka kwamba wasomi, maulama wa kidini, wanasiasa na viongozi wa nchi za Kiislamu wanabeba sehemu muhimu zaidi ya majukumu na mapambano hayo matakatifu ya yenye mwisho na hatima njema.

Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa: Mwenyezi Mungu ameahidi kusaidia na kunusuru mapambano haya, na mkutano wenu huu ni sehemu ya harakati hiyo kuu na adhimu.

Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Muungano wa Maulama wa Muqawama huko Lebanon ulioanza leo utakamilisha kazi zake kesho tarehe Pili Novemba. 

Sheikh Maher Hammoud amesema Mkutano wa Pili wa Muungano wa Kimataifa wa Maulama wa Muqawama mjini Beirut unafanyika sambamba na kutimia miaka mia moja tangu kulipotolewa Azimio la Balfour tarehe Pili Novemba 1917. Ameongeza kuwa lengo la mkutano huo ni kukumbusha suala muhimu kwamba, Palestina ndilo suala muhimu zaidi katika eneo la Mashariki ya Kati. 

Kaulimbinu ya mkutano huo ni: "Ahadi ya Balfour hadi ahadi ya Mwenyezi Mungu".

Azimio hilo ambalo liliwasilishwa na Arthur Balfour  Waziri wa Mambo ya Nje wa wakati huo wa Uingereza, liliandaa uwanja wa kuasisiwa utawala wa Kizayuni wa Israel huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu. 

3658985


captcha