IQNA

Mfumo wa Sauti katika Masjid Nabawi waimarishwa kwa kutumia teknolojia ya nano

20:05 - November 05, 2017
Habari ID: 3471249
TEHRAN (IQNA)-Chuo Kikuu cha Taibah nchini Saudi Arabia kimefanikiwa kutumia teknolojia ya nano kuimarisha mfumo wa vipaza sauti katika Al-Masjid an-Nabawi (Msikiti wa Mtume SAW) mjini humo.

Dkt. Wasim A. Orfali Mkuu Kitivo cha Uhandisi katika Chuo Kikuu cha Taibah cha Madina amesema mfumo wa vipaza sauti katika Masjid Nabawi umeimarishwa kwa kutegemea teknolojia ya nano.

Amesema chuo hicho kwa ushirikiano na taasisi za kigeni wameweza kutumia mbinu erevu ili kuboresha viwango vya vipaza sauti katika msikiti huo.

Dkt. Orfali amesema lengo la kutumia teknolojia ya nano ili sauti iweze kuenda sambamba na mwanga, joto na unyevu wa hewa. Kwa kuzingatia vipimo hivyo,  vipaza sauti vinaeneza sauti katika katika maeneo mbali mbali ya msikiti kwa mlingano ulio sahihi na wenye utulivu kwa msikilizaji.

Nano ni teknolojia mpya inayohusu matumizi ya vitu vidogo sana na miundo yake ambayo inapimwa kuwa kati ya nanomita 1-100.

Asili ya Nano ni nanomita ambayo ni kipimo cha sehemu ya bilioni moja ya mita. Hii inamaanisha vitu ambavyo ni vikubwa kuliko atomi na vidogo mara 1000 kuliko upana wa unywele.

3660381

captcha