IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
10:59 - December 13, 2018
News ID: 3471769
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, maadui wamefeli katika njama ya maadui wa Iran ya kuwachoche baadhi ya watu kufanya maandamano mitaani na kuyapa jina la "Majira ya Joto Kali".

Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameyasema hayo Jumatano mjini Tehran katika hotuba yake kwenye hadhara ya familia za mashahidi wa vita vya kujitetea kutakatifu, Walinzi wa Haram na mipaka ya Iran. Ayatullah Khamenei aliashiria harakati za miaka miwili ya hivi karibuni za Marekani hususan kuweka vikwazo vya pande zote na kuwasaidia maadui dhidi ya Iran na kusema mipango na njama zao zimefichuka. Amesisitiza kuwa, lengo lao lilikuwa kuzusha migawanyiko, hitilafu na vita baina ya makundi mbalimbali nchini kupitia njia ya vikwao na kuhujumu usalama wa Iran, na vilevile kuwachoche baadhi ya watu kufanya maandamano mitaani na kuyapa jina la "Majira ya Joto Kali", lakini kinyume cha matakwa hayo ya adui, majira ya joto ya mwaka huu yalikuwa miongoni mwa misimu bora zaidi ya joto hapa nchini.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu pia ameashiria matamshi yaliyotolewa na maafisa wa serikali ya Marekani wakidai kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitauona mwaka wake wa 40 na kusema: Taifa la Iran limeendelea kusimama kidete, na kwa taufiki yake Mwenyezi Mungu, tarehe 22 Bahman (Februari 11) litaadhimisha mwaka wa 40 wa Mapinduzi ya Kiislamu katika sherehe kubwa na adhimu kuliko miaka iliyopita.

Ayatullah Ali Khamenei amewataja Wazayuni na tawala zilizobakia nyuma katika eneo la Asia Magharibi kuwa ni washirika wa Marekani katika kupanga njama dhidi ya taifa la Iran na kusema kuwa, Iran ni imara na yenye nguvu kubwa zaidi kuliko wao kwani hadi sasa hawajaweza kufanya lolote na wala hawataweza.

Baraka za Uislamu

Amelitaka taifa la Iran kuwa macho kikamilifu na kufuatilia hali ya mambo kwa umakini mkubwa na kusema kuwa: Katika dunia ya sasa iliyokumbwa ya tufani ambayo imefika hadi Ulaya na Ufaransa, taifa la Iran limepanda meli ya kuwapenda Ahul Bayt wa Mtume Muhammad SAW kwa baraka ya Uislamu na hatimaye litaibuka na ushindi.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, maadui mashuhuri wa Iran ya Kiislamu wameghariki katika ufisadi wa kimaadili na kisiasa na kwamba, kama unataka kuijua vyema Marekani watazame viongozi na rais wa nchi hiyo.

Ameongeza kuwa, viongozi wa Marekani wanaabudu pesa na hawajali uhai na mali ya wanadamu na mfano wa wazi wa ukweli huo ni Yemen ambako Wasaudia wanafanya jinai na mauaji, na Wamarekani ndio washirika wao.

Amesema Wasaudia wakishirikiana na Marekani wanashambulia hospitali, masoko na maeneo yenye idadi kubwa ya watu; hawa ni watenda jinai na hii ndiyo sura halisi ya Marekani.

3771828

Name:
Email:
* Comment: