IQNA

Utawala wa Israel wamkamata Mkuu wa Wakfu katika mjini Quds

11:30 - February 25, 2019
Habari ID: 3471852
TEHRAN (IQNA)- Askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamemkamata mkuu wa Idara ya Wakfu inayosimamia maeneo matakatifu ya Kiislamu katika mji wa Quds (Jerusalem) .

Kwa mujibu wa taarifa, Sheikh Abdul Azim Salhab, mkurugenzi wa Idara ya Wakfu katika mji wa Quds alikmatwa mapema Jumapili kama sehemu ya oparesheni zilizotekelezwa na wanajeshi wa utawala haramu wa Israel katika maeneo ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Quds ambayo yote yanakaliwa kwa mabavu na utawala huo ghasibu wa Israel.

Wakuu wa utawala wa Kizayuni walimuahili huru Sheikh Azim Salhab kufuatia mashinikizo. Hatahvyo kukamatwa mwanazuoni huo wa Kiislamu ni jambo lisilo la kawaida kwani yeye ni raia wa Jordan. Kwa kawaida iwapo wakuu wa utawala wa Kizayuni walilenga kumsaili mkuu wa wakfu walikuwa wanamuita katika ofisi zao lakini mara hii wamepata kiburi zaidi na kumvunjia heshima kwa kumkamata. Wapalestina wanasema kumkamata mwanazuoni huyo mwenye umri wa miaka 75 ni jambo lisilokubalika.

Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu Jordan Sheikh Abdul Nasser Abu al-Basal  amelaani vikali kukamatwa Sheikh Salhab na kusema utawala wa Kizayuni wa Israel unacheza na moto katika mazingira magumu.

Wapalestina wazuiwa kusali Al Aqsa

Siku ya Jumatatu wiki iliyopita, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel walikuwa wameufunga mlango wa Bab al Rahman a kuwazuia Wapalestina kuingia katika Msikiti wa Al Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu.

Utawala haramu wa Israel unauvunjia heshima Msikiti wa Al Aqsa katika hali ambayo watawala wa nchi za Kiarabu wakiongozwa na Saudi Arabia wana uhusiano wa siri na Israel na wako mbioni kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala huo unaokalia kwa mabavu qibla cha kwanza cha Waislamu na ardhi za jadi za Wapalestina.

Hivi karibuni Ismail Haniya, Mkuu wa Idara ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, HAMAS, ametoa taarifa na kusema "Hatua za Wazayuni katika mji unaokaliwa kwa mabavu wa Quds ikiwa ni pamoja na kufunga lango la Bab al Rahma na pia kuzuia kazi za baadhi ya miasasa ya Al Aqsa ni jambo linaloonyesha wazi lengo lao la kuweka masharti mapya katika kuugawa msikiti huo na kueneza satwa yao katika msikiti huo."

Kongamano la Warsaw lazidisha kiburi cha Israel

Kiongozi wa HAMAS ameendelea kusema hujuma mpya na hatari ya Wazayuni dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa imeanza baada ya Kongamano la Warsaw kwa sababu wakuu wa utawala ghasibu wanadhani kongamano hilo limeibua mgawanyiko katika nchi za Kiarabu kuhusu kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni.

Kati ya malengo makuu ya Kongamano la Warsaw ni kudhoofisha muqawama au harakati za ukombozi Mashariki ya Kati na kuendeleza mchakato wa nchi za Kiarabu kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel sambamba na kuainisha ramani mpya ya satwa ya Marekani na Israel Mashariki ya Kati.

Kongamano la Warsaw la Februari 13 na 14 lilikuwa sawa na idhini ya Marekani kwa Israel izidishe njama zake dhidi ya Ulimwengu wa Kiislamu na hivyo hatua ya Israel ya kukithirisha uchochezi wake katika Msikiti wa Al Aqsa inaweza kutathminiwa katika fremu hiyo.

Njama dhidi ya Al Aqsa

Kiujumla mipango na harakati za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya msikiti wa Al-Aqsa kama za kuugawa msikiti huo mtakatifu kiwakati na kimahali zinafanyika katika fremu ya mipango hatari ya utawala huo vamizi yenye lengo la kujitanua katika eneo la Mashariki ya Kati.

Katika miaka ya hivi karibuni wakuu wa utawala wa Kizayuni wamekithirisha njama zao za kuugawa msikiti wa Al Aqsa kiwakati na kimahali na sasa kadiri muda unavyosonga mbele ndivyo njama hizo za kuutekea msikiti huo zinavyoshika kasi huku haki za Wapalestina zikikandamizwa.

Kwa mtazamo wa kiwakati, kwa muda wa takribani siku 200 kwa mwaka, utawala wa Kizayuni wa Israel huwazuia Waislamu kuingia katika Msikiti wa Al Aqsa. Kwa mtazamo wa kimahali pia, utawala ghasibu wa Israel hivi sasa umeteka na kuwakabidhi Wazayuni asilimia 60 ya eneo lote la Msikiti wa Al Aqsa.

3467992/

captcha