IQNA

Wiki ya kuujua Uislamu yazinduliwa Montreal, Canada

10:30 - January 25, 2020
Habari ID: 3472404
TEHRAN (IQNA) – 'Wiki ya Kuujua Uislamu' imezinduliwa katika mji wa Montreal nchini Canada ambapo washiriki wametafakari kuhusu tukio ambalo lillijiri katika Msikiti wa Mji wa Quebec miaka mitatu iliyopita.

"Kwetu sisi ni wiki muhimu sana kwa sababu harakati ii ilianza Januari 29 2017," amesema Boufeldja Benabdalla, muasisi wa Kituo cha Kiislamu cha Quebec.

Itakumbukwa kuwa mnamo Januari 29 2017 Msikiti wa Quebec ulihujumiwa na magaidi ambapo  Waislamu sita waliuawa katika hujuma ya kigaidi. Magaidi waliwafyatulia risasi Waislamu waliokuwa katika msikiti wa Kituo cha Kiutamaduni cha Quebec, wakati wa Sala ya Ishaa saa mbili usiku.

Tukio hilo lilikumbukwa mwaka uliofuata lakini washiriki wakataka kuchukuliwe hatua zaidi ili kuelimisha jamii kuhusu Waislamu na Uislamu na kwa msingi huo, 'Wiki ya Kuujua Uislamu' ikaanzishwa mwaka 2019 ili kuleta maelewano baina ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu.

Wiki hiyo inaadmishiwa kuanzia Januari 25-31 na kuna harakati kadhaa zikiwemo makongamano, maoneysho ya  filamu, na mijadala. Misikiti mingi mjini Montreal imesema itaweka milango yake wazi kwa wasiokuwa Waislamu.

Kwa ujumla Canada ni nchi ambayo huwakaribisha wahamiaji na wafuasi wa dini zote lakini katika miaka ya hivi karibuni kumeshuhudiwa ongezeko la vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.

3470432

captcha