IQNA

Misikiti Singapore yaungana katika kutoa futari

14:42 - May 09, 2020
Habari ID: 3472749
TEHRAN (IQNA) – Misikiti 37 nchini Singapore imeungana na kuchanga dola laki sita kwa ajili ya kutoa futari kwa Waislamu wanaofunga saumu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kwa mujibu wa mpango huo, vifurushi 20,000 vya futari vitasambazwa kila siku kwa wafanyakazi wa sekta za afya na familia  zao, watu ambao kawaida hupokea Zaka na familia zinginezo ambazo zinahitaji msaada katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Mbasi na msaada huo ambo umetolewa na misikiti, kwa ujumla mchango wa Ramadhani nchini Singapore ambao umekabidhiwa mfuko wa SGUnited Buka Puasa umefika dola milioni 2.58.

Kwa kuzingatia kuwa misiki ya Singapore imefungw akwa muda ili kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19, mwaka huu hakuna mpango wa kuwalisha watu futari na hivyo fedha  zilizochangwa zimekabidhiwa moja kwa moja kwa wanaohitajia.

Singapore au Singapuri ni nchi ndogo na iliyostawi katika Asia ya Kusini-Mashariki ambayo uchumi wake unategemea zaidi biashara, hasa benki pamoja na viwanda. Waislamu wanakadiriwa kuwa asilimia 15 ya watu wote milioni 5.6.

3897456

captcha