Ujumbe huo ukiongozwa na Mitja Leskovar, Balozi wa Vatican nchini Iraq aliyekuwa akimuwakilisha Papa Francis, ulifika Najaf Alhamisi na kukutana na viongozi wa ngazi za juu wa Kiislamu kwa lengo la kujadili safari tarajiwa ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki nchini Iraq.
Ujumbe huo ulitembelea maeneo mbali mbali ya Haram ya Imam Ali AS na kupata maelezo kuhusu yanayojiri katika eneo hilo takatifu alipozikwa Imam Ali AS.
Papa Francis anatazamiwa kutembelea Iraq Machi 5 kwa lengo la kukutana na viongozi wa nchi hiyo ya Kiarabu ambapo pia atakutana na kiongozi wa ngazi za juu wa Kiislamu Ayatullah Ali al-Sistani.