IQNA

Imam wa muda wa Sala ya Ijumaa ya hapa mjini Tehran

Marekani haina nia ya kufanya mazungumzo, bali inachopigania ni wizi tu

18:46 - January 28, 2022
Habari ID: 3474862
TEHRAN (IQNA)- Imam wa muda wa Sala ya Ijumaa ya hapa mjini Tehran amegusia mazungumzo yanayoendelea mjini Vienna kuhusu kuondolewa vikwazo vya kidhulma ilivyowekewa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema kuwa, Marekani ina wajibu wa kuondoa vikwazo vyote ilivyoiwekea Iran, tena kwa sura ya kudumu.

Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesema hayo katika khutba za Sala ya Ijumaa ya leo ya mkoa wa Tehran na kuongeza kuwa, Marekani haina nia ya kufanya mazungumzo, bali inachopigania ni wizi tu. Muda wote Marekani inaota kuiba na kupora mali za mataifa mengine lakini ndoto hiyo ya Marekani haijawahi kuaguka na kamwe haitoaguka mbele ya Iran.

Imam huyo wa muda wa Sala ya Ijumaa ya Tehran ameashiria pia maafa ya kibinadamu yanayofanywa na wavamizi nchini Yemen na kusema, Saudi Arabia inawashambulia mtawalia kwa mabomu wananchi wa Yemen, jinai hiyo inauma sana, lakini kinachoumiza zaidi ni kuona mashirika na taasisi za kimataifa ukimwemo Umoja wa Mataifa bali hata taasisi za kimataifa za Waislamu zimenyamaza kimya kabisa mbele ya jinai za wavamizi wa Yemen.

Vile vile amesema, pamoja na yote lakini, kuna jambo la kujivunia nalo ni kwamba muqawama wa wananchi Waislamu na wanajihadi wa Yemen unaendelea kufelisha njama za maadui.

Kwa mwaka wa nane sasa wananchi hao wanaendelea kupambana kiume na kishujaa na si tu wamefanikiwa kumrudisha nyuma adui, lakini pia wameuthibitishia ulimwengu kuwa, taifa la Yemen ni taifa asili ambalo linastahiki kusifiwa na kupongezwa.

4031930

captcha